📰 Newspapers

Mbadi, Mwanasheria Mkuu hatarini kuadhibiwa kwa kukosa kufichua mikataba ya mikopo ya Serikali

Mbadi, Mwanasheria Mkuu hatarini kuadhibiwa kwa kukosa kufichua mikataba ya mikopo ya Serikali

WAZIRI wa Fedha John Mbadi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dorcas Oduor wameamriwa kufika katika Mahakama Kuu Novemba 27, 2026, kusikilizwa kabla ya kupewa adhabu kwa kupuuza amri za mahakama kuhusu ufichuzi wa mikataba ya mikopo ya kimataifa.

Jaji Patricia Nyaundi aliwapata wawili hao na hatia ya kudharau mahakama baada ya serikali kukosa kutoa maelezo kuhusu mikopo ya kimataifa na jinsi fedha hizo zilivyotumika.

Jaji alisema wawili hao watawasilisha sababu za kupunguziwa adhabu kabla ya hukumu kutolewa.

Kesi hiyo inatokana na uamuzi wa Desemba 2024 ambapo Mahakama Kuu iliamua kuwa serikali ilikiuka haki ya wananchi kupata habari kwa kukataa kutoa maelezo kuhusu mikopo kwa kipindi cha miaka tisa.

Jaji Lawrence Mugambi aliamuru serikali kutoa stakabadhi hizo ndani ya siku 45 kufuatia ombi la Tume ya Haki za Kibinadamu Kenya na Wanjiru Gikonyo.

Jaji Nyaundi alisema ushahidi ulionyesha kuwa amri ya mahakama ilifikishwa kwa maafisa hao, lakini hawakuwasilisha majibu kupinga ombi la kuwatangaza kuwa walidharau mahakama.

Alionya kuwa amri za mahakama ni lazima ziheshimiwe na kwamba kuziacha kukiukwa bila hatua kunadhoofisha utawala wa sheria.

In brief

WAZIRI wa Fedha John Mbadi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dorcas Oduor wameamriwa kufika katika Mahakama Kuu Novemba 27, 2026, kusikilizwa kabla ya kupewa adhabu kwa kupuuza amri za mahakama kuhusu ufichuzi wa mikataba ya mikopo ya kimataifa. Jaji Nyaundi alisema ushahidi ulionyesha kuwa amri ya mahakama ilifikishwa kwa maafisa hao, lakini hawakuwasilisha majibu kupinga ombi la kuwatangaza kuwa walidharau mahakama.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.