Joho, Mvurya wapambania kudhibiti Kwale

Joho, Mvurya wapambania kudhibiti Kwale

USHINDANI wa kuwania ugavana Kwale kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027 unazidi kuonekana kama mchuano wa kisiasa kati ya Waziri wa Madini na Uchumi wa Baharini, Bw Hassan Joho wa ODM, na mwenzake wa Michezo, Bw Salim Mvurya wa UDA.

Bw Mvurya anaongoza juhudi za kuhakikisha kaunti hiyo inasalia chini ya UDA huku Bw Joho akitangaza nia ya ODM kuendeleza ushawishi wake katika eneo la Pwani.

“Ni lazima tukifanye ODM kuwa imara tena. Hatuwezi kuruhusu vyama vingine kuchukua maeneo yaliyokuwa ya ODM,” alisema Bw Joho wakati wa mkutano wa hivi majuzi wa kisiasa Kwale.

Gavana Fatuma Achani, ambaye anatumikia muhula wake wa kwanza, anakabiliwa na ushindani mkali baada ya waliokuwa wakimezea mate tikiti ya ODM, Profesa Hamadi Boga na mfanyabiashara Lungazi Mangale, kuamua kuungana ili kumuunga mkono mmoja wao.

Wawili hao, walioibuka wa pili na wa tatu mtawalia katika uchaguzi wa 2022, wamehimizwa na viongozi wa mashinani kudumisha ushirikiano wao hadi uchaguzi utakapofanyika.

Viongozi wa ODM wameonya kuwa kuvunjika kwa muungano huo kunaweza kudhoofisha azma ya chama hicho ya kutwaa kiti cha ugavana.

Licha ya mikakati hiyo inayoendelea, Waziri Mvurya amewataka wapinzani wa Bi Achani kujiandaa kwa mchuano mkali unaofanana na uchaguzi mdogo wa Msambweni wa mwaka 2020.

Uchaguzi huo ulikuwa kipimo kikubwa cha ushawishi wa kisiasa kati yake na Waziri Joho, ambao wakati huo walikuwa magavana wa Kwale na Mombasa…

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics

Help us understand visits and countries – anonymous and aggregated.

Marketing

Used to measure and personalise adverts and social media content.