Winnie njiapanda kisiasa uchaguzi wa 2027 ukijongea

Winnie njiapanda kisiasa uchaguzi wa 2027 ukijongea

MBUNGE wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Winnie Odinga, anakabiliwa na utata kuhusu upande wa kisiasa wa kuegemea anapotafuta kiti cha useneta Nairobi katika Uchaguzi Mkuu wa 2027.

Winnie ameshindwa kuweka wazi iwapo anaunga mkono uongozi wa ODM au vuguvugu la Linda Mwananchi.

Kutokuwepo kwake katika mikutano miwili muhimu Ijumaa na Jumamosi Nairobi kumezidisha maswali kuhusu mwelekeo wake wa kisiasa.

Winnie hakuhudhuria uzinduzi wa makao makuu ya Linda Mwananchi jijini Nairobi wala mkutano wa ODM katika uwanja wa Jacaranda ulioongozwa na viongozi wakuu wa chama hicho.

Katika kuwatambulisha viongozi wa Linda Mwananchi uliofanyika Lavington Ijumaa, kiti cha mbele kilikuwa kimetengewa Winnie, lakini hakufika.

Hali hiyo inatatanisha zaidi kwa sababu Oktoba 15, wakati wa kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo cha baba yake Raila Odinga, Winnie alitangaza kuwania useneta Nairobi akisema anataka kufanya hivyo pamoja na vijana.

“Najua watu wengi wamekuwa wakiuliza nilipo na ninakoelekea. Leo nataka kuwajibu ili kuondoa uvumi,” akasema.

“Kwa kuwa Edwin Sifuna anawania wadhifa mwingine, nafasi ya useneta Nairobi iko wazi. Ndiyo maana nimeamua kuwania kiti hicho. Siendi pekee yangu, ninaenda na vijana,” akaongeza.

Matamshi hayo yalifasiriwa kuwa anaegemea Linda Mwananchi, lakini kutohudhuria uzinduzi wake kumezua maswali zaidi.

Hata ndani ya vuguvugu hilo, Winnie anakabiliwa na ushindani kutoka kwa Seneta Maalum, Crystal Asige, ambaye amekuwa akiandamana na Bw Sifuna katika ziara zake za kisiasa.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics

Help us understand visits and countries – anonymous and aggregated.

Marketing

Used to measure and personalise adverts and social media content.