Rekodi ya maendeleo itampa Ruto Tutam 2027 – Kindiki

Rekodi ya maendeleo itampa Ruto Tutam 2027 – Kindiki

NAIBU Rais Profesa Kithure Kindiki anatumia mafanikio ya serikali ya Kenya Kwanza katika sekta mbalimbali kuimarisha uungwaji mkono wa Rais William Ruto, huku akiweka msingi wa kusalia katika wadhifa huo kampeni za uchaguzi za 2027 zikichacha.

Katika kipindi cha miaka miwili tangu achukue nafasi ya Rigathi Gachagua, Profesa Kindiki amejitahidi kuonyesha mchango wake katika kuleta udhabiti serikalini akiratibu utekelezaji wa miradi muhimu.

Juhudi zake pia zinaonekana kulenga kuimarisha uungwaji mkono wa Rais Ruto katika ukanda wa Mlima Kenya, ambao ni muhimu katika mipango ya Rais kutafuta muhula wa pili.

Katika tathmini ya utendaji wa serikali, Profesa Kindiki alitetea rekodi ya utawala huo akisema umepiga hatua kubwa licha ya ukosoaji kutoka kwa wapinzani.

“Utawala wa Ruto umefanya vizuri zaidi ya matarajio yaliyowekewa, lakini wakosoaji hawatoi tathmini ya haki kuhusu utendakazi wake. Ukosoaji wao una nia mbaya na hauna ukweli,” akasema.

Alitaja kilimo kama mojawapo ya sekta ambazo serikali imepiga hatua, akisema wakulima milioni 7.9 wa mimea na wafugaji milioni tatu wamesajiliwa ili kurahisisha mipango na utoaji wa huduma.

“Leo tunajua tuna wakulima wangapi, mifugo waliyo nayo, wanakoishi, mazao wanayolima na aina ya mbolea wanayohitaji,” akasema.

Prof Kindiki alisema bei ya gunia la kilo 50 la mbolea imepungua kutoka Sh7,000 mnamo 2022 hadi Sh2,000. Bei ya mbegu bora za mahindi pia imeshuka kutoka Sh300 hadi Sh150 kwa kilo moja.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics

Help us understand visits and countries – anonymous and aggregated.

Marketing

Used to measure and personalise adverts and social media content.