Mustakabali wa Carrick kuamuliwa katika kikao Monaco

Mustakabali wa Carrick kuamuliwa katika kikao Monaco

MUSTAKABALI wa kocha wa Manchester United, Michael Carrick, utaamuliwa leo, katika kikao kitakachohudhuriwa na mmiliki wa klabu hiyo Sir Jim Ratcliffe pamoja na viongozi wakuu Omar Berrada na Jason Wilcox mjini Monaco.

Kibarua cha Carrick kiko hatarini baada ya United kushuka hadi nafasi ya 18 kwenye jedwali la Ligi Kuu UIngereza (EPL) kufuatia sare ya 4-4 dhidi ya Aston Villa Jumapili.

Kwa mujibu wa BBC Sport, Berrada, ambaye ni mtendaji mkuu, na Wilcox, mkurugenzi wa soka, wanatarajiwa kumshauri Ratcliffe na familia ya Glazer kumtimua kocha huyo.

Hata hivyo, uamuzi wa mwisho huenda ukafanywa kesho. Kikao hicho kilikuwa kimepangwa awali na hakikuandaliwa mahsusi kujadili hatma ya Carrick, ingawa suala lake linatarajiwa kutawala mazungumzo.

Pia, kutajadiliwa uwezekano wa kuongeza makocha katika benchi yake ya ufundi.

Iwapo uamuzi wa kumtimua utafikiwa, United watamwelezea Carrick ana kwa ana.

United walianza vibaya zaidi msimu wa ligi ya nyumbani katika kipindi cha miaka 40, wakiwa na ushindi mmoja pekee katika mechi 10 za EPL. Wamefungwa mabao 19, huku wakiwa pointi moja pekee juu ya Crystal Palace wanaoshikilia mkia.

Sare dhidi ya Aston Villa ilikuwa mechi ya tatu ya Carrick tangu klabu hiyo iamue kumpa muda zaidi kubasilisha matokeo. Katika mechi hizo, alipata ushindi mmoja, sare moja na kupoteza nyingine.

Uongozi wa United ulifikiria kumfuta kazi baada ya kichapo cha 3-0 dhidi ya Bournemouth, lakini ukaamua kumpa…

In brief

MUSTAKABALI wa kocha wa Manchester United, Michael Carrick, utaamuliwa leo, katika kikao kitakachohudhuriwa na mmiliki wa klabu hiyo Sir Jim Ratcliffe pamoja na viongozi wakuu Omar Berrada na Jason Wilcox mjini Monaco. Sare dhidi ya Aston Villa ilikuwa mechi ya tatu ya Carrick tangu klabu hiyo iamue kumpa muda zaidi kubasilisha matokeo. Katika mechi hizo, alipata ushindi mmoja, sare moja na kupoteza nyingine.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics

Help us understand visits and countries – anonymous and aggregated.

Marketing

Used to measure and personalise adverts and social media content.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.