Gavana Rotich akashifiwa kwa kumdhalilisha naibu wake, Prof Cheserek

Gavana Rotich akashifiwa kwa kumdhalilisha naibu wake, Prof Cheserek

VIONGOZI wanawake katika eneo la North Rift wamemkashifu Gavana wa Elgeyo Marakwet Wesley Rotich kwa madai ya kumdhalilisha naibu wake Profesa Grace Cheserek katika hafla ya umma.

Tukio hilo lilitokea Kapyego, wadi ya Marakwet Mashariki, wakati gavana alipojaribu kunyakua kipaza sauti kutoka kwa Prof Cheserek alipokuwa akihutubia wakazi.

Hata hivyo, naibu huyo alikataa kuondoka jukwaani, akisisitiza kuwa alikuwa na haki ya kuzungumza.

“Wacha nimalize hotuba yangu, Gavana. Si wewe uliyenialika hapa. Nitaendelea kuzungumza na nitasema yote,” alisema.

Mvutano huo ulizidi huku Prof Cheserek akikosoa serikali ya kaunti kwa kushindwa kutoa huduma muhimu, hasa katika sekta za afya na elimu.

Pia aliishutumu kwa kuzingatia zaidi kugawa misaada ili kupata uungwaji mkono wa kisiasa badala ya kutafuta suluhu ya kudumu kwa matatizo ya wakazi.

Gavana alikerwa na matamshi hayo na kuelekeza walinzi wake kumuondoa naibu wake jukwaani.

Video ya tukio hilo ilisambaa mitandaoni na kuzua mjadala kuhusu heshima kwa wanawake waliochaguliwa kushikilia nyadhifa za uongozi.

Akizungumza akiwa Eldoret, Benadine Korir wa Muungano wa Kutetea Haki za Wanawake, alisema tukio hilo linaonyesha kutoheshimiwa kwa wanawake katika uongozi.

Alisema Prof Cheserek alichaguliwa na wananchi na anastahili kuheshimiwa anapotekeleza majukumu yake.

Bi Jane Lengut wa Chama cha Wanawake katika Siasa, alisema tabia hiyo inaweza kufuta hatua zilizopigwa kuhakikisha wanawake wanapata nafasi katika uongozi.

In brief

VIONGOZI wanawake katika eneo la North Rift wamemkashifu Gavana wa Elgeyo Marakwet Wesley Rotich kwa madai ya kumdhalilisha naibu wake Profesa Grace Cheserek katika hafla ya umma. Gavana alikerwa na matamshi hayo na kuelekeza walinzi wake kumuondoa naibu wake jukwaani. Akizungumza akiwa Eldoret, Benadine Korir wa Muungano wa Kutetea Haki za Wanawake, alisema tukio hilo linaonyesha kutoheshimiwa kwa wanawake katika uongozi.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics

Help us understand visits and countries – anonymous and aggregated.

Marketing

Used to measure and personalise adverts and social media content.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.