Ruto ataka vijana wamuunge mkono, asema atang’atuka awaachie serikali 2032

Ruto ataka vijana wamuunge mkono, asema atang’atuka awaachie serikali 2032

RAIS William Ruto amewataka vijana kumuunga mkono akidai viongozi wa upinzani wamekuwa mamlakani kwa miaka mingi bila kuleta mabadiliko.

Akiendeleza ziara yake katika eneo la Gusii kwa siku ya tatu, Dkt Ruto aliwashambulia viongozi hao akiwalaumu kwa kuwazuia wanasiasa vijana wanaochipuka wakihofia kupoteza ushawishi wao.

Rais aliahidi kuwa ifikapo 2032, ataachia kizazi kipya cha viongozi nafasi ya kuongoza nchi.

“Nyinyi vijana na mimi, hawa wote ni watu wa rika langu. Ninawahakikishia vijana kwamba nitawaweka pamoja viongozi hawa na kuhakikisha tunaondoka mamlakani 2032 ili kukabidhi nchi kwa vijana,” alisema.

Hakuwataja viongozi aliowalenga kwa majina, badala yake akatumia majina ya utani kuwakosoa.

Alitaja wabunge vijana kama Osoro wa South Mugirango na Zaheer Jhanda wa Nyaribari Chache, akisema wanapaswa kuachwa wakue kisiasa bila kuandamwa na wapinzani wao.

Alidai baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwapiga vita wanasiasa chipukizi wakiwemo John Methu, Ndindi Nyoro, Kimani Ichung’wah na Aaron Cheruiyot.

Rais pia aliwahimiza vijana wa Gusii kujisajili katika mpango wa NYOTA ili kunufaika na nafasi za kujiajiri na kukuza biashara zao.

Alisema serikali yake imezalisha nafasi za ajira kupitia miradi mbalimbali, ikiwemo nyumba za gharama nafuu, ajira nje ya nje na kazi za kidijitali.

Kwa mujibu wake, mradi wa nyumba za gharama nafuu umezalisha ajira milioni 1.1, huku Wakenya 680,000 wakipata kazi nje ya nchi na wengine 350,000 wakijipatia riziki kupitia kazi za kidijitali.

In brief

RAIS William Ruto amewataka vijana kumuunga mkono akidai viongozi wa upinzani wamekuwa mamlakani kwa miaka mingi bila kuleta mabadiliko. Rais aliahidi kuwa ifikapo 2032, ataachia kizazi kipya cha viongozi nafasi ya kuongoza nchi. Ninawahakikishia vijana kwamba nitawaweka pamoja viongozi hawa na kuhakikisha tunaondoka mamlakani 2032 ili kukabidhi nchi kwa vijana,” alisema. Hakuwataja viongozi aliowalenga kwa majina, badala yake akatumia majina ya utani kuwakosoa.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.