Makosa ya ngono yasababisha maelfu ya wanaume kusota jela

Makosa ya ngono yasababisha maelfu ya wanaume kusota jela

TAKRIBAN mfungwa mmoja kati ya watatu waliohukumiwa nchini Kenya ni mwanamume anayetumikia kifungo gerezani kwa makosa ya kingono, huku ubakaji wa watoto ukiongoza kwa idadi kubwa ya hukumu hizo.

Ripoti mpya inaonyesha kuwa wafungwa 11,108 kati ya takriban 37,000 waliohukumiwa wako gerezani kwa makosa yanayohusiana na ukatili wa kingono.

Hii ni sawa na asilimia 31 ya wafungwa wote waliohukumiwa.

Kati ya makosa hayo, ubakaji wa watoto unachangia asilimia 78.3, ukifuatiwa na ubakaji wa watu wazima kwa asilimia 10, kujamiiana na ndugu wa karibu kwa asilimia 6.1 na makosa mengine ya kingono kwa asilimia 5.6.

Takwimu hizo zimeangaziwa katika ripoti ya mwaka wa fedha wa 2025/2026 kuhusu usimamizi wa haki, iliyotolewa wiki iliyopita na Jaji Mkuu Martha Koome kupitia Baraza la Kitaifa la Usimamizi wa Haki (NCAJ).

Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa visa 32,694 vya ukatili wa kijinsia viliripotiwa nchini katika kipindi hicho, huku Nairobi ikiongoza kwa idadi ya visa vilivyosajiliwa.

Kaunti nyingine zilizorekodi visa vingi ni Meru, Nakuru, Kiambu na Machakos.

Ubakaji wa watoto uliendelea kuwa kosa la kingono lililoripotiwa zaidi, huku visa 5,823 vikirekodiwa kote nchini.

Nairobi ilirekodi visa 3,004 vya ukatili wa kijinsia, vikiwemo 363 vya ubakaji wa watoto, 79 vya ubakaji, 47 vya unyanyasaji wa kingono na 52 vya vitendo vya aibu vya kingono.

In brief

TAKRIBAN mfungwa mmoja kati ya watatu waliohukumiwa nchini Kenya ni mwanamume anayetumikia kifungo gerezani kwa makosa ya kingono, huku ubakaji wa watoto ukiongoza kwa idadi kubwa ya hukumu hizo. Kati ya makosa hayo, ubakaji wa watoto unachangia asilimia 78.3, ukifuatiwa na ubakaji wa watu wazima kwa asilimia 10, kujamiiana na ndugu wa karibu kwa asilimia 6.1 na makosa mengine ya kingono kwa asilimia 5.6. Ubakaji wa watoto uliendelea kuwa kosa la kingono lililoripotiwa zaidi, huku visa 5,823 vikirekodiwa kote nchini.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.