Matumaini mvua inayonyesha itaimarisha uzalishaji maziwa na kupunguza bei

Matumaini mvua inayonyesha itaimarisha uzalishaji maziwa na kupunguza bei

WAKENYA wana matumaini kuwa bei ya maziwa itapungua katika wiki zijazo kutokana na mvua inayoendelea kunyesha katika maeneo mengi nchini.

Matumaini ya wengi ni kuwa mvua inatarajiwa kuongeza upatikanaji wa malisho na uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Kwa miezi kadhaa sasa, uhaba wa maziwa uliochangiwa na ukame wa muda mrefu na ukosefu wa malisho umesababisha bei kupanda kutoka Sh50 hadi Sh85 kwa lita.

Wengi wanasema gharama hiyo ya juu imewalazimu kubadili matumizi yao ya kila siku, huku wengine wakipunguza kiasi cha maziwa wanachonunua ili kukabiliana na hali ngumu ya maisha.

Kwa familia nyingi, kupanda kwa bei hakukuathiri tu unywaji wa chai, bali pia bajeti ya kununua bidhaa nyingine muhimu za nyumbani.

Hata hivyo, wana matumaini kuwa mvua za Novemba na Desemba zitasaidia wakulima kupata malisho ya kutosha na kuongeza uzalishaji.

Wanasema upatikanaji wa nyasi na malisho mengine karibu na mashamba utapunguza pia gharama ya kuyasafirisha kutoka maeneo ya mbali, ambayo imechangia kuongeza gharama ya uzalishaji wa maziwa.

Kwa upande mwingine, wauzaji wa maziwa wameathiriwa na uhaba huo baada ya baadhi ya wateja kupunguza ununuzi kutokana na bei ya juu.

Wauzaji hao wanasema biashara zao zilidorora tangu Julai, wakati wakulima walipoanza kupunguza kiasi cha maziwa walichokuwa wakisambaza kutokana na ukame.

Baadhi ya wakulima waliokuwa wakisambaza hadi lita 100 kwa siku walipunguza kiasi hicho hadi lita 50 au 60.

In brief

WAKENYA wana matumaini kuwa bei ya maziwa itapungua katika wiki zijazo kutokana na mvua inayoendelea kunyesha katika maeneo mengi nchini. Matumaini ya wengi ni kuwa mvua inatarajiwa kuongeza upatikanaji wa malisho na uzalishaji wa bidhaa hiyo. Hata hivyo, wana matumaini kuwa mvua za Novemba na Desemba zitasaidia wakulima kupata malisho ya kutosha na kuongeza uzalishaji.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.