Weather across Africa

Mhubiri aagizwa kumlipa mkewe wa zamani Sh900,000 kwa kufichua hali yake ya HIV

Mhubiri aagizwa kumlipa mkewe wa zamani Sh900,000 kwa kufichua hali yake ya HIV

JOPO la Masuala ya Ukimwi limeagiza mwanamume aliyefichua hali ya afya ya aliyekuwa mkewe kwa jamaa, waumini wa kanisa na wanajamii bila idhini yake kumlipa fidia ya Sh900,000.

Mahakama hiyo ilipata kuwa mwanamume huyo, ambaye ni mhubiri, alikiuka haki ya mwanamke huyo ya kutunza siri za taarifa zake za kiafya na kumsababishia maumivu ya kisaikolojia.

Katika uamuzi wake, mahakama pia ilimzuia mwanamume huyo kufichua tena hali ya Ukimwi ya aliyekuwa mkewe.

Mwanamke huyo, aliyetambuliwa kwa herufi LGG, aliwasilisha kesi Mei 25, 2026, dhidi ya aliyekuwa mumewe GMM, akimlaumu kwa kusambaza taarifa kuhusu hali yake ya HIV bila idhini yake.

Alitaka alipwe fidia kutokana na ubaguzi, unyanyasaji wa kisaikolojia, kudhalilishwa na kupoteza mapato. Alisema vitendo hivyo vilimfanya akumbwe na unyanyapaa, aibu na msongo wa mawazo.

Wawili hao walikuwa wameoana na kupata watoto watatu kabla ya kutalikiana mwaka 2016.

LGG aliambia mahakama kuwa alikuwa amemsaidia mumewe kifedha na kihisia alipokuwa akiendelea na masomo yake, huku akigharamia mahitaji ya familia.

Hata hivyo, alisema uhusiano wao ulianza kuzorota baada ya kugunduliwa kuwa na virusi vya HIV.

Kwa mujibu wa ushahidi wake, mumewe alianza kumwambia kuwa angekufa hivi karibuni kutokana na virusi hivyo. Pia alidai kuwa alitishiwa kunyimwa pesa na mali kwa sababu ya hali yake ya afya.

LGG alidai kuwa aliyekuwa mumewe alimnyima msaada wa kifedha, akaingilia kazi yake na kutumia hali yake ya…

In brief

JOPO la Masuala ya Ukimwi limeagiza mwanamume aliyefichua hali ya afya ya aliyekuwa mkewe kwa jamaa, waumini wa kanisa na wanajamii bila idhini yake kumlipa fidia ya Sh900,000. Katika uamuzi wake, mahakama pia ilimzuia mwanamume huyo kufichua tena hali ya Ukimwi ya aliyekuwa mkewe. LGG alidai kuwa aliyekuwa mumewe alimnyima msaada wa kifedha, akaingilia kazi yake na kutumia hali yake ya…

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.