Kazi ya uuguzi haijamzuia kuendeleza ufugaji kijijini

Kazi ya uuguzi haijamzuia kuendeleza ufugaji kijijini

MWENDO wa saa kumi na moja alfajiri wakati kijiji cha Nyatike, eneobunge la Mugirango Kusini, Kaunti ya Kisii, bado kimetulia, shughuli katika banda la nguruwe la Mary Kwamboka Nyakwara huwa tayari zimeamza.

Akiwa ameshika ndoo ya kijani yenye Azolla mbichi na nyingine ya mabuu ya Black Soldier Fly (BSF), Mary huingia zizini kuwalisha nguruwe wake sita.

Anawaita kwa majina, nao huitikia kwa milio ya furaha.

“Nguruwe wanajua sauti ya mama yao. Wakisikia tu hatua zangu, wanaanza kulia kwa furaha,” anasema huku akitabasamu.

Kwa Mary, huu ni utaratibu wa kila asubuhi kabla ya kuvaa sare nyeupe na kuelekea kazini kama muuguzi katika kituo cha afya mjini Suneka.

Ufugaji wa nguruwe ni biashara yake ya ziada, lakini anasema umegeuka kuwa uwekezaji muhimu unaomsaidia kugharamia mahitaji ya familia na elimu ya watoto.

“Shamba langu liko Nyatike, kazi yangu iko Suneka. Asubuhi niko shambani, mchana niko wodini, na jioni narudi tena kuangalia mifugo wangu,” anasema.

Ili kuhakikisha shughuli za shamba zinaendelea wakati hayupo, Mary amemwajiri Philip Ochieng', mwanafunzi aliyehitimu mafunzo ya afya ya mifugo kutoka Chuo Anuwai cha Kisii, kuwa meneja wa shamba.

Kwa sasa, Mary anafuga nguruwe sita aliowachagua kwa umakini: majike matano aina ya Large White na dume mmoja aina ya Duroc kwa ajili ya uzalishaji.

“Sita bora ni bora kuliko 20 wasiofaa. Namjua kila mmoja kwa jina, uzito wake na mahitaji…

In brief

MWENDO wa saa kumi na moja alfajiri wakati kijiji cha Nyatike, eneobunge la Mugirango Kusini, Kaunti ya Kisii, bado kimetulia, shughuli katika banda la nguruwe la Mary Kwamboka Nyakwara huwa tayari zimeamza. “Shamba langu liko Nyatike, kazi yangu iko Suneka. Asubuhi niko shambani, mchana niko wodini, na jioni narudi tena kuangalia mifugo wangu,” anasema. Ili kuhakikisha shughuli za shamba zinaendelea wakati hayupo, Mary amemwajiri Philip Ochieng', mwanafunzi aliyehitimu mafunzo ya afya ya mifugo kutoka Chuo Anuwai cha Kisii, kuwa meneja wa shamba.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.