Guinnea Bissau sasa yakubali kuchunguza mauaji ya mwanaharakati Vigario Luis Balanta

Guinnea Bissau sasa yakubali kuchunguza mauaji ya mwanaharakati Vigario Luis Balanta

BISSAU, Guinea Bissau: KIONGOZI Mkuu wa Mashtaka Guinea-Bissau ameunda kamati ya kuchunguza mauaji ya msanii wa nyimbo za kufokafoka na mwanaharakati Vigario Luis Balanta kufuatia shinikizo kutoka kwa upinzani na vyombo vya habari kutaka waliohusika wawajibishwe.

Balanta aliuawa Machi baada ya awali kueleza hofu kuwa maisha yake yalikuwa hatarini. Mauaji yake yalisababisha wanachama wa vuguvugu la kijamii na kisiasa aliloanzisha, Po' di Terra wajifiche.

Vuguvugu hilo limeishutumu serikali inayoongozwa na wanajeshi kwa kuwalinda waliohusika na mauaji hayo.

Serikali hiyo ilitwaa mamlaka kupitia mapinduzi ya kijeshi mnamo Novemba 2025. Hata hivyo, awali ililaani mauaji ya Balanta na kusema haiwezi kutoa maelezo zaidi hadi uchunguzi ukamilike.

Katika taarifa Jumatatu, afisi ya mwendesha mashtaka ilisema kamati hiyo itakuwa na siku 60 kubaini washukiwa, makosa yaliyotendwa na kuwasilisha matokeo ya uchunguzi.

Po' di Terra ilikaribisha hatua hiyo Jumanne, lakini ikataka uchunguzi huru, wa kina na ulio wazi kwa umma.

“Kamati hii ni ishara kwamba shinikizo la wananchi na matakwa ya kupata ukweli hayawezi kupuuzwa,” taarifa ya vuguvugu hilo ilisema.

Kiongozi mpya wa vuguvugu hilo, Nado da Cunha, alisema wataendelea kudai haki.

“Tunataka kamati hii isitumiwe kujinufaisha kisiasa au kuboresha taswira kuhusu taasisi za serikali,” alisema katika ujumbe kutoka Brazil, anakokaa kwa sababu za kiusalama.

In brief

BISSAU, Guinea Bissau: KIONGOZI Mkuu wa Mashtaka Guinea-Bissau ameunda kamati ya kuchunguza mauaji ya msanii wa nyimbo za kufokafoka na mwanaharakati Vigario Luis Balanta kufuatia shinikizo kutoka kwa upinzani na vyombo vya habari kutaka waliohusika wawajibishwe. Vuguvugu hilo limeishutumu serikali inayoongozwa na wanajeshi kwa kuwalinda waliohusika na mauaji hayo. Hata hivyo, awali ililaani mauaji ya Balanta na kusema haiwezi kutoa maelezo zaidi hadi uchunguzi ukamilike.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.