Viongozi maarufu wa siasa wavua vazi la heshima na kurushina majina ya kudhalilishana

Viongozi maarufu wa siasa wavua vazi la heshima na kurushina majina ya kudhalilishana

SIASA za Kenya zinazidi kutawaliwa na vijembe, majina ya kejeli na mashambulizi binafsi huku viongozi wakionekana kutumia muda mwingi kushambuliana badala ya kueleza mipango yao ya kuboresha maisha ya wananchi.

Mvutano huo umeongezeka kati ya Rais William Ruto na aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagua, huku kila mmoja akimtupia mwenzake tuhuma na majina ya kumdhalilisha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.

Katika ziara yake ya siku tatu eneo la Gusii, Ruto alimlaumu Gachagua kwa kuwatoza kwa vitisho fedha wafanyabiashara, magavana na wanaotaka tiketi za chama chake cha DCP ili kuwapa tiketi na hata kuzungumza katika mikutano ya kisiasa.

Hakutoa ushahidi wa kuthibitisha madai hayo.

Gachagua alijibu kwa kejeli, akisema Rais amekuwa akitoa ahadi za maendeleo Kisii na Nyamira bila kutekeleza miradi inayotarajiwa.

Alisema yeye si barabara, mradi wa maji wala uwanja wa ndege kuzungumziwa katika mikutano ya rais eneo hilo.

Ruto baadaye alimwita Gachagua “Bwana Texas”, akirejelea kauli ya aliyekuwa naibu rais kwamba atahamia Amerika iwapo Ruto atachaguliwa tena.

Hata hivyo, wachambuzi wanasema majina hayo ya kejeli yanaweza kuficha tofauti kati ya tuhuma, ukweli uliothibitishwa na matusi ya kisiasa.

Mwanaharakati Boniface Mwangi anasema wananchi hawapaswi kufurahia matusi pekee, bali kuchunguza madai yanayotolewa na viongozi na kutaka ushahidi.

Analaumu pia vyombo vya habari na umma kwa kupatia nafasi kubwa kauli zinazozua burudani huku ajenda za maendeleo zikisahaulika.

In brief

SIASA za Kenya zinazidi kutawaliwa na vijembe, majina ya kejeli na mashambulizi binafsi huku viongozi wakionekana kutumia muda mwingi kushambuliana badala ya kueleza mipango yao ya kuboresha maisha ya wananchi. Mvutano huo umeongezeka kati ya Rais William Ruto na aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagua, huku kila mmoja akimtupia mwenzake tuhuma na majina ya kumdhalilisha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Ruto baadaye alimwita Gachagua “Bwana Texas”, akirejelea kauli ya aliyekuwa naibu rais kwamba atahamia Amerika iwapo Ruto atachaguliwa tena.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.