Iran yakwamilia madini ya nyuklia, yaambia Amerika ikiichokoza tena ‘itakipata’

Iran yakwamilia madini ya nyuklia, yaambia Amerika ikiichokoza tena ‘itakipata’

TEHRAN, Iran: IRAN imesema haitaruhusu hata chembe kimoja cha madini yake ya nyuklia yaliyorutubishwa kusafirishwa nje ya nchi na kuonya kuwa Amerika itakabiliwa vikali iwapo itafanya mashambulizi mengine dhidi yake.

Mkuu wa masuala ya usalama Iran, Mohsen Rezaei, alisema hayo katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Al Mayadeen cha Lebanon kinachounga mkono Iran.

Kauli yake inajiri wakati maafisa wa Amerika wanapunguza shinikizo za kutaka hatua zaidi za kijeshi zichukuliwe dhidi ya Iran.

Wachanganuzi wanasema Rais Donald Trump amekuwa akitumia lugha ya adabu na kutuma ishara ya maridhiano tangu chama chake cha Republican kishindwe katika uchaguzi wa katikati ya muhula uliofanyika Novemba 3.

Rezaei alisema hakuna mazungumzo yanayoendelea kwa sasa kati ya Tehran na Washington.

“Shambulizi lolote jipya la Amerika litajibiwa kwa kulenga vituo vyake vya kijeshi vilivyo mbali,” akasema.

Aliongeza kuwa Kiongozi Mkuu wa Dini Iran Mojtaba Khamenei ametoa amri kuwa urani iliyokaribia kiwango cha kutumika kutengeneza silaha za nyuklia isisafirishwe nje ya nchi.

Maafisa wawili wakuu wa Iran walithibitisha mnamo Mei kuwa kulikuwa na agizo hilo.

“Tunahitaji madini hayo yaliyorutubishwa ili kutengeneza meli zinazotumia nyuklia,” akasema Rezaei.

Aliongeza kuwa Tehran tayari imeifahamisha Moscow kuwa madini hayo yatasalia Iran na kwamba serikali itayatumia yenyewe.

Urusi ilikuwa imejitolea kuondoa urani Iran kama sehemu ya makubaliano yanayoweza kupunguza wasiwasi wa Amerika kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran.

In brief

TEHRAN, Iran: IRAN imesema haitaruhusu hata chembe kimoja cha madini yake ya nyuklia yaliyorutubishwa kusafirishwa nje ya nchi na kuonya kuwa Amerika itakabiliwa vikali iwapo itafanya mashambulizi mengine dhidi yake. “Tunahitaji madini hayo yaliyorutubishwa ili kutengeneza meli zinazotumia nyuklia,” akasema Rezaei. Aliongeza kuwa Tehran tayari imeifahamisha Moscow kuwa madini hayo yatasalia Iran na kwamba serikali itayatumia yenyewe.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.