MJANE wa aliyekuwa waziri mkuu marehemu Raila Odinga, Ida Odinga, ameweka wazi msimamo wake wa kisiasa baada ya wiki kadhaa za minong’ono kuhusu mwelekeo wa familia yake kutokana na kifo cha mumewe.
Ida amesema bado yuko katika chama cha ODM na anaunga mkono Serikali Jumuishi inayoongozwa na Rais William Ruto, akisisitiza kuwa huo ndio msimamo ambao Raila alimwachia kabla ya kufariki.
Akizungumza Jumanne, Novemba 10, katika uzinduzi wa mpango wa usimamizi wa eneo la Gembe Hills, eneobunge la Suba Kaskazini, Ida alisema hana nia ya kuachana na misingi ya kisiasa ya mumewe.
“Aliponiacha, hapo ndipo nilipo. Aliniacha katika ODM na Serikali Jumuishi na bado nimesimama hapo,” alisema.
Aliongeza kuwa Raila alimweleza kuwa Dkt Ruto ndiye kiongozi wa nchi na kwamba huo ndio msimamo ambao alipaswa kuendeleza.
Kauli hii inajiri wiki kadhaa baada ya familia ya Odinga kukosolewa kwa kuwaalika viongozi wa mirengo tofauti ya kisiasa kwenye hafla ya Oktoba 15 katika uwanja wa Migwena, Bondo, kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha Raila.
Miongoni mwa walioalikwa alikuwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa Raila.
Ingawa hakuhudhuria, viongozi wengine wa upinzani, akiwemo Kalonzo Musyoka, Edwin Sifuna, Martha Karua na Jimi Wanjigi, walihudhuria.
Hatua hiyo iliwakera baadhi ya viongozi wa ODM.
Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa, Junet Mohamed, alisema alikosa hafla hiyo baada ya kuona jina la…