RAIS William Ruto na kiongozi wa Linda Mwananchi Edwin Sifuna sasa wanatoshana kwa umaarufu katika kinyang'anyiro cha urais, hali inayoashiria ushindani mkali katika Uchaguzi Mkuu wa 2027, kwa mujibu wa utafiti mpya.
Utafiti uliofanywa na kampuni ya TIFA ambao ulitolewa jana, ulionyesha kuwa viongozi hao wawili wanaungwa mkono na asilimia 31 kila mmoja, na kwa sasa hakuna mshindi anayeweza kufikisha asilimia 50.
Kwa mujibu wa TIFA, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka ana asilimia tisa, akifuatwa na Naibu Kiongozi wa Jubilee, Dkt Fred Matiang’i kwa asilimia tano huku aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua akiwa na asilimia nne.Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo hayo jijini Nairobi, Mtafiti wa TIFA Tom Wolf alisema umaarufu wa Bw Sifuna umeongezeka kwa kasi tangu alipoondoka ODM na kuwa kiongozi wa Linda Mwananchi.
“Umaarufu wa Bw Sifuna umeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu apate chama cha kisiasa, ikilinganishwa na tafiti za awali alipokuwa bado ndani ya ODM,” akasema Wolf.Umaarufu wa Bw Sifuna umeongezeka kutoka asilimia 10 mnamo Mei hadi asilimia 15 Julai, kabla ya kufikia asilimia 31 katika utafiti uliotangazwa jana uliofanywa kati ya Oktoba 6 na Novemba 11.
Kwa upande wake, Rais Ruto pia amepiga hatua, akipanda kutoka asilimia 24 mnamo Mei na Julai hadi asilimia 31.Umaarufu wake umeongezeka kutoka asilimia 18 aliyokuwa nayo Agosti mwaka jana.“Katika hali hii, Rais Ruto na Bw Sifuna wameimarisha umaarufu wao…