📰 Newspapers

ODM ilivyotumia ujanja kufunika UDA katika ziara ya Ruto eneo la Gusii

ODM ilivyotumia ujanja kufunika UDA katika ziara ya Ruto eneo la Gusii

ZIARA ya siku nne ya Rais William Ruto katika kaunti za Kisii na Nyamira wiki hii, imefichua ushindani unaozidi kuongezeka kati ya chama chake cha United Democratic Alliance (UDA) na mshirika wake katika serikali jumuishi, Orange Democratic Movement (ODM).

Wafuasi wa UDA walidai kutishwa na kushambuliwa na makundi ya vijana wanaodaiwa kuhusishwa na mwanasiasa wa eneo hilo, katika juhudi za kuonyesha kuwa Kisii ni ngome ya ODM.Hali ilizidi kuwa mbaya katika eneo bunge la Bonchari, ambapo wafuasi wa mwakilishi wa kike Kisii, Doris Aburi, walidaiwa kunyanyaswa.

Mbunge huyo pia alizomewa na baadaye kukosa kuhudhuria mikutano mingine ya Rais, hasa iliyofanyika mjini Kisii.Baada ya vurugu hizo, Rais Ruto anaripotiwa kukutana na viongozi wa ODM nyumbani kwake Kilgoris Jumatano jioni, kujadili mvutano huo. Waliohudhuria ni Gladys Wanga, Abdulswamad Shariff Nassir, Hassan Joho na msaidizi wa Rais, Farouk Kibet.

Gavana wa Mombasa, Bw Nassir, baadaye alichapisha mitandaoni kuhusu mashauriano hayo.Wakati wa mikutano hiyo, Gavana wa Kisii na naibu kiongozi wa ODM, Simba Arati, alifafanua msimamo wa chama chake kuhusu ushirikiano na UDA.Alisema wakazi wa Kisii wataendelea kumuunga mkono Rais Ruto kwa kuwa ODM inaamini kuwa serikalini kutaisaidia kuleta maendeleo.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa ODM haitaingia katika makubaliano ya kisiasa na UDA kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027 bila masharti yanayolinda maslahi yake.Alisema chama hicho lazima kijadiliane na kupata masharti yaliyo wazi na yenye manufaa.…

In brief

ZIARA ya siku nne ya Rais William Ruto katika kaunti za Kisii na Nyamira wiki hii, imefichua ushindani unaozidi kuongezeka kati ya chama chake cha United Democratic Alliance (UDA) na mshirika wake katika serikali jumuishi, Orange Democratic Movement (ODM). Wafuasi wa UDA walidai kutishwa na kushambuliwa na makundi ya vijana wanaodaiwa kuhusishwa na mwanasiasa wa eneo hilo, katika juhudi za kuonyesha kuwa Kisii ni ngome ya ODM.Hali ilizidi kuwa mbaya katika eneo bunge la Bonchari, ambapo wafuasi wa mwakilishi wa kike Kisii, Doris Aburi, walidaiwa kunyanyaswa.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.