📰 Newspapers

Hospitali zitatozwa faini ya Sh2 milioni kwa kuzuilia wagonjwa, miili

Hospitali zitatozwa faini ya Sh2 milioni kwa kuzuilia wagonjwa, miili

Wasimamizi wa hospitali za umma na kibinafsi watatozwa faini ya hadi Sh2 milioni kwa kuwazuilia wagonjwa wanaopaswa kuruhusiwa kuondoka au miili ya marehemu kwa sababu ya madeni ya matibabu.

Hatua hiyo imependekezwa katika Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Afya wa 2024, ambao umepitishwa kwa kauli moja na wabunge na sasa unasubiri kutiwa saini na Rais William Ruto ili kuwa sheria.

Mswada huo uliodhaminiwa na Mwakilishi wa Wanawake wa Kirinyaga, Njeri Maina, unamulika hospitali zinazokataa kumhudumia mgonjwa au kumzuia kuondoka kwa sababu hajalipa bili au ameshindwa kutoa amana ya matibabu.

Pia unakataza hospitali kuzuilia miili ili kulazimisha familia kulipa gharama za matibabu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Bunge, James Nyikal, alisema sheria hiyo itasaidia familia maskini ambazo zimekuwa zikiteseka baada ya wapendwa wao kuzuiliwa hospitalini kutokana na madeni.

Mbunge wa Mwingi Magharibi Charles Ngunya alihoji sababu za hospitali kuzuilia miili ya marehemu, akisema kitendo hicho si cha kiafya.

Hata hivyo, mswada huo unaruhusu hospitali kuwataka wagonjwa au jamaa zao kutia saini hati ya ahadi ya kulipa deni kabla ya mgonjwa au mwili kuruhusiwa kuondoka.

Hati hiyo itaeleza muda na utaratibu wa kulipa deni na itakuwa na nguvu ya kisheria, hivyo hospitali zinaweza kuishtaki familia isipotimiza ahadi.

In brief

Wasimamizi wa hospitali za umma na kibinafsi watatozwa faini ya hadi Sh2 milioni kwa kuwazuilia wagonjwa wanaopaswa kuruhusiwa kuondoka au miili ya marehemu kwa sababu ya madeni ya matibabu. Pia unakataza hospitali kuzuilia miili ili kulazimisha familia kulipa gharama za matibabu. Hata hivyo, mswada huo unaruhusu hospitali kuwataka wagonjwa au jamaa zao kutia saini hati ya ahadi ya kulipa deni kabla ya mgonjwa au mwili kuruhusiwa kuondoka.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.