JOPO la kushughulikia masuala ya Ukimwi limeamuru shule moja ya sekondari Kaunti ya Kajiado pamoja na mkuu wake kumlipa mwanafunzi fidia ya Sh1.2 milioni kwa kufichua hali yake ya afya bila idhini yake.
Mahakama hiyo ilibaini kuwa mkuu huyo alikiuka haki ya mwanafunzi huyo ya faragha na kumbagua kutokana na hali yake ya kiafya, hali iliyochangia kuondoka kwake shuleni baada ya kukumbwa na unyanyapaa.
Mwanafunzi huyo, aliyetambuliwa kama D.N katika kesi hiyo, alisema walimu walifichua hali yake kwa wanafunzi wengine bila idhini yake. Pia alidai mkuu wa shule aliwaambia wazazi wake wamchukue kwa sababu alikuwa na virusi vya ukimwi.
Alisimulia kuwa matatizo yalianza alipoingia katika chumba cha walimu baada ya kumaliza adhabu na kuwakuta wakijadili hali yake ya kiafya.Mmoja wa walimu alimwuliza iwapo alikuwa amemeza dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV).
Alisema aliposikia mazungumzo hayo aliondoka shuleni na kwenda kuishi na dada yake. Alipojaribu kurejea, shule ilikataa kumpokea.Mama yake alisema mkuu wa shule alimweleza kwa simu kuwa mwanafunzi huyo alikuwa ametoroka. Katika mazungumzo yaliyofuata, mkuu huyo alimwambia aende kumchukua kwa sababu alikuwa na Ukimwi na hakutaka aendelee kusoma shuleni hapo.
Baba yake pia alidai aliulizwa na mkuu huyo: “Unajua mtoto wako ako na ukimwi?”Dada ya mwanafunzi huyo aliambia jopo kuwa mkuu wa shule alimwita mwanafunzi wa kiume aliyekuwa akihusishwa kimapenzi na dada yake na kumuuliza kama alijua…