📰 Newspapers

Wanalala kazini majengo yakiendelea kuporomoka na kuua watu nchini

Wanalala kazini majengo yakiendelea kuporomoka na kuua watu nchini

Vifo vya watu sita baada ya jengo la ghorofa nane kuporomoka likiendelea kujengwa kando ya Barabara ya Mombasa jijini Nairobi jana, vimeibua tena maswali kuhusu usalama wa majengo na uwajibikaji katika sekta ya ujenzi nchini.

Watu wengine watano walijeruhiwa katika mkasa huo uliotokea Ijumaa eneo la Syokimau, huku maafisa zikisema watu wote 405 waliokuwa katika eneo la ujenzi walikuwa wamepatikana.

Msaidizi wa Inspekta Jenerali wa Polisi anayesimamia masuala ya majanga, Duncan Ochieng, alisema miili sita ilipatikana na majeruhi watano kupelekwa katika Hospitali ya Imara Daima.

Wahudumu wa zimamoto wa Kaunti ya Nairobi na kikosi cha uokoaji walitumwa eneo hilo kupekua vifusi na kuhakikisha hakuna watu waliokuwa wamenasa.

Huu ni mkasa wa pili mkubwa wa aina hiyo katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja. Mnamo Oktoba 23, jengo la ghorofa 18 liliporomoka Eastleigh, Nairobi, na kuua watu wanane huku wengine wakiripotiwa kutoweka.

Takwimu za Wizara ya Ardhi, Kazi za Umma, Nyumba na Maendeleo ya Miji zinaonyesha kuwa majengo 100 yameporomoka nchini katika kipindi cha miaka 30 iliyopita. Zaidi ya watu 40 wamefariki kutokana na mikasa hiyo katika miaka mitano iliyopita.

Mwaka 2022 ulirekodi visa vingi zaidi, majengo 13 yaliporomoka. Mwaka 2021 na 2023 kila mmoja ulirekodi visa 12, huku 2018 ukiwa na visa tisa. Mwaka 2015 na 2019 kila mmoja ulirekodi majengo saba kuporomoka.

In brief

Vifo vya watu sita baada ya jengo la ghorofa nane kuporomoka likiendelea kujengwa kando ya Barabara ya Mombasa jijini Nairobi jana, vimeibua tena maswali kuhusu usalama wa majengo na uwajibikaji katika sekta ya ujenzi nchini. Watu wengine watano walijeruhiwa katika mkasa huo uliotokea Ijumaa eneo la Syokimau, huku maafisa zikisema watu wote 405 waliokuwa katika eneo la ujenzi walikuwa wamepatikana. Mwaka 2015 na 2019 kila mmoja ulirekodi majengo saba kuporomoka.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.