📰 Newspapers

Mackenzie asubiri hukumu zaidi baada ya kusukumwa jela miaka 200

Mackenzie asubiri hukumu zaidi baada ya kusukumwa jela miaka 200

Hata baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 200 gerezani pasta Paul Mackenzie bado anaandamwa na kivuli cha maafa ya Shakahola,

Licha ya kuandika historia nchini Kenya kwa kuhukumiwa kifungo kirefu kiasi hicho, hukumu hiyo haijamaliza masaibu yake mahakamani.

Bado anakabiliwa na kesi nyingine zinazotokana na vifo vya zaidi ya wafuasi 450 wa kanisa lake la Good News International Ministries (GNI).

Mackenzie alihukumiwa kifungo cha miaka 200 gerezani Novemba 6 baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya watu 191, wakiwemo watoto 190.

Hata hivyo, anakabiliwa na hukumu nyingine tatu katika kesi tofauti zinazohusiana na mkasa wa Shakahola.

Hukumu ya kwanza inatarajiwa kutolewa Novemba 24 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mombasa, katika kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili Mackenzie na washtakiwa wenzake 95, kuhusiana na vifo vya watu 238.

Upande wa mashtaka unadai kuwa washtakiwa hao walishirikiana kutekeleza makubaliano ya pamoja ya kujiua, yaliyosababisha vifo vya watu hao katika msitu wa Shakahola kati ya Januari 2021 na Septemba 2023.

Novemba 25, Mahakama ya Watoto ya Tononoka inatarajiwa kutoa uamuzi katika kesi ya kuwatesa watoto, ambapo Mackenzie na washirika wake 34 wanakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na ukatili, mateso na kuwanyima watoto haki ya kupata elimu.

Upande wa mashtaka unadai kuwa watoto waliondolewa shuleni, wakalazimishwa kufunga na kunyimwa mahitaji ya kimsingi. Baadhi yao walipigwa walipopinga mafundisho hayo au kujaribu kutoroka.

In brief

Hata baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 200 gerezani pasta Paul Mackenzie bado anaandamwa na kivuli cha maafa ya Shakahola, Licha ya kuandika historia nchini Kenya kwa kuhukumiwa kifungo kirefu kiasi hicho, hukumu hiyo haijamaliza masaibu yake mahakamani. Hata hivyo, anakabiliwa na hukumu nyingine tatu katika kesi tofauti zinazohusiana na mkasa wa Shakahola. Hukumu ya kwanza inatarajiwa kutolewa Novemba 24 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mombasa, katika kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili Mackenzie na washtakiwa wenzake 95, kuhusiana na vifo vya watu 238.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.