📰 Newspapers

Ukaguzi waanika wanafunzi 800,000 na shule 200 hewa

Ukaguzi waanika wanafunzi 800,000 na shule 200 hewa

Ukaguzi wa serikali katika sekta ya elimu umegundua kuwa sajili za shule za msingi zilikuwa na majina ya wanafunzi hewa wapatao 800,000 na karibu shule 200 ambazo hazipo.

Ufichuzi huo umeibua maswali kuhusu jinsi fedha za serikali za kugharamia elimu zilivyokuwa zikitolewa kwa shule bila kuthibitisha idadi halisi ya wanafunzi.

Rais William Ruto alisema ukaguzi huo wa kitaifa ulifichua udhaifu katika mifumo ya Wizara ya Elimu ya kukusanya na kuhakiki takwimu za wanafunzi.Wizara ilikuwa na mifumo mitatu tofauti ya kidijitali iliyotumiwa na wakuu wa shule, wakurugenzi wa elimu wa kaunti na maafisa wa makao makuu kuwasilisha taarifa.

Wakuu wa shule waliwasilisha idadi ya wanafunzi na maelezo ya taasisi zao, huku wakurugenzi wa elimu wakikusanya takwimu zao ili kulinganisha na kubaini tofauti. Hata hivyo, mifumo iliyotumiwa na maafisa wa mashinani haikuunganishwa, hivyo kulazimisha maafisa kulinganisha taarifa hizo kwa mikono.

Kufikia Novemba 10, 2025, shule 44,495 zilikuwa zimeidhinishwa kupokea fedha kulingana na idadi ya wanafunzi iliyothibitishwa.

Nyingine 4,555 zilipata nusu ya fedha zilizoonyesha katika rekodi za awali, huku shule 5,851 zikilipwa kulingana na idadi iliyobainika.Wakati huo, shule 1,005 za msingi na za sekondari msingi zilikuwa na taarifa zisizo sahihi au hazikuwasilisha data.

Wizara ilieleza Kamati ya Bunge kuhusu Hesabu za Umma Februari 24, 2026 kuwa, wakuu wa shule 20 walikuwa wameripotiwa kwa Tume ya Huduma za Walimu (TSC) kuchukuliwa hatua za kinidhamu…

In brief

Ukaguzi wa serikali katika sekta ya elimu umegundua kuwa sajili za shule za msingi zilikuwa na majina ya wanafunzi hewa wapatao 800,000 na karibu shule 200 ambazo hazipo. Ufichuzi huo umeibua maswali kuhusu jinsi fedha za serikali za kugharamia elimu zilivyokuwa zikitolewa kwa shule bila kuthibitisha idadi halisi ya wanafunzi. Kufikia Novemba 10, 2025, shule 44,495 zilikuwa zimeidhinishwa kupokea fedha kulingana na idadi ya wanafunzi iliyothibitishwa.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.