📰 Newspapers

Matiang’i arejea Gusii baada ya Ruto, asema wakazi hawawezi kununuliwa kwa pesa

Matiang’i arejea Gusii baada ya Ruto, asema wakazi hawawezi kununuliwa kwa pesa

Siku mbili baada ya Rais William Ruto kukamilisha ziara yake ya siku nne eneo la Gusii, mgombeaji urais wa Jubilee, Dkt Fred Matiang’i, amerejea katika eneo hilo akisema ziara ya Rais haitabadilisha msimamo wa kisiasa wa jamii ya Abagusii.

Matiang’i alisema wakazi wamechoshwa na ahadi ambazo anadai hazijatekelezwa na serikali ya Rais Ruto, hivyo hawako tayari kuachana na upinzani kwa sababu ya fedha au zawadi wanazopewa na wanasiasa.

Akikosoa ziara ya Rais, aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani alisema siasa za Kenya zimegeuzwa kuwa mnada ambako viongozi wenye fedha nyingi wanadhani wanaweza kununua uungwaji mkono wa wananchi.

“Mioyo, nafsi na dhamiri za watu wetu wa Gusii haziuzwi. Rais alikuwa hapa mapema wiki hii akigawa pesa, kama inavyoonekana katika video zinazosambaa mitandaoni. Watu wetu hawawezi kununuliwa,” alisema.

Alisema wananchi wanataka maendeleo halisi na kuboreshwa kwa maisha yao, badala ya viongozi kujaribu kuwashawishi kwa hongo na ahadi zisizotekelezwa.

Matiang’i alisema hayo Ijumaa alipohudhuria mazishi ya mjomba wake, Mzee John Mboga Nyaboga, eneo la Manga, eneobunge la Borabu, Kaunti ya Nyamira.

Alisema hatamjibu Rais kwa matusi, akisisitiza kuwa kampeni zinapaswa kufanywa kwa heshima bila vitisho wala vurugu. Pia aliunga mkono wito wa maaskofu Katoliki wa kuwepo kwa kampeni za amani na umoja.

Kiongozi huyo wa Jubilee alikosoa serikali kwa kile alichokitaja kuwa ufisadi na kushindwa kudhibiti wizi wa mifugo katika eneo la Gusii.

In brief

Siku mbili baada ya Rais William Ruto kukamilisha ziara yake ya siku nne eneo la Gusii, mgombeaji urais wa Jubilee, Dkt Fred Matiang’i, amerejea katika eneo hilo akisema ziara ya Rais haitabadilisha msimamo wa kisiasa wa jamii ya Abagusii. Watu wetu hawawezi kununuliwa,” alisema. Alisema hatamjibu Rais kwa matusi, akisisitiza kuwa kampeni zinapaswa kufanywa kwa heshima bila vitisho wala vurugu.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.