WAZIRI wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku na Mbunge wa Kasarani Ronald Karauri wanajiandaa kukabiliana katika mchujo wa UDA kuwania ugavana wa Nairobi 2027, hali ambayo ni mtihani kwa Rais William Ruto kudhibiti ushindani wa kisiasa ndani ya chama chake.
Wawili hao wanataka kumrithi Gavana Johnson Sakaja, aliyehama UDA na kujiunga na ODM.
Bw Ruku anajitambulisha kama msimamizi mwenye uzoefu, huku Bw Karauri akijenga kampeni yake kwa kudai kazi yake Kasarani inaonekana.
Bw Karauri alipokelewa rasmi UDA Novemba 9 na viongozi wakuu wa chama, akiwemo Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah na Katibu Mkuu Hassan Omar.
Bw Ichung’wah alifichua kuwa Rais Ruto alikuwa amempigia simu na kumwelekeza ampokee mbunge huyo.
Bw Ichung’wah pia alimtaja Karauri kuwa mgombea wa chama atakayekabiliana na ODM Nairobi, hatua iliyozua hisia kuwa huenda anapendelewa dhidi ya wagombea wengine.
Hata hivyo, Bw Ruku amesema anajitambulisha na UDA licha ya kuwa alichaguliwa bungeni kupitia DP kabla ya kujiuzulu na kuwa waziri.
“Rais amebadilisha nchi hii na ninakubaliana kikamilifu na misingi ya UDA. Ndiyo maana ninawania kiti hicho kupitia tiketi ya UDA,” akasema.
Alipoulizwa iwapo amezungumza na Rais kuhusu kuondoka serikalini na kuwania ugavana, alijibu: “Tumwache Rais nje ya mazungumzo haya.”
Bw Ruku amekuwa akifanya mikutano na wakazi wa Nairobi, akisema amekuwa akiishi jijini humu tangu akiwa na umri wa miaka 18 na watoto wake…