📰 Newspapers

Kosovo, mtaa mdogo wenye makanisa 50! ‘Ikifika Jumapili, kelele hazivumiliki’

Kosovo, mtaa mdogo wenye makanisa 50! ‘Ikifika Jumapili, kelele hazivumiliki’

KATIKA eneo la Makanisani, maarufu kama Kosovo, lililoko Uthiru mpakani mwa Nairobi na Kiambu, kuna hali ya kipekee ambapo zaidi ya makanisa 50, makazi na biashara ndogo ndogo zimesongamana kwenye kipande kidogo cha ardhi katikati ya Barabara Kuu ya Waiyaki Way.

Eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 1.75 lina nyumba 135, nyingi zikiwa zimejengwa kwa mabati. Kosovo inafanana na mtaa wa mabanda.

Baadhi ya wakazi wameishi hapo kwa miongo kadhaa, huku familia nyingine zikiwa na vizazi vitatu vinavyoishi katika eneo hilo.

Hata hivyo, makanisa ndiyo yanayotawala mandhari ya Kosovo, huku mengine yakiwa yamejengwa kwa kubanana kiasi kwamba nafasi kati ya majengo mawili ni chini ya sentimita moja.

Bw Josh Adom, ambaye amekuwa akiishi eneo hilo tangu 1986, anakumbuka wakati ambapo kulikuwa na makanisa machache na sehemu kubwa ya ardhi ilikuwa na miti na mimea.

“Nilipofika hapa, makanisa yalikuwa machache na sehemu iliyobaki ilikuwa kama shamba au msitu,” akasema.

Kwa mujibu wa Bw Adom, Kanisa la Hebron Church of Africa, linalohusishwa na waumini wa Akorino, ndilo lilikuwa la kwanza kuanzishwa eneo hilo.

Anaongeza kuwa serikali ilijenga vibanda sawia na vilivyo katika soko la Uthiru, vikitenganishwa na seng’enge, lakini wafanyabiashara walipokosa kuvitumia, baadhi ya watu walifunika mianya katika seng’enge hizo na kuanza kuishi humo.

Baadaye, makanisa yakaanza kuchipuka.

In brief

KATIKA eneo la Makanisani, maarufu kama Kosovo, lililoko Uthiru mpakani mwa Nairobi na Kiambu, kuna hali ya kipekee ambapo zaidi ya makanisa 50, makazi na biashara ndogo ndogo zimesongamana kwenye kipande kidogo cha ardhi katikati ya Barabara Kuu ya Waiyaki Way. “Nilipofika hapa, makanisa yalikuwa machache na sehemu iliyobaki ilikuwa kama shamba au msitu,” akasema.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.