KAMPALA, Uganda:
MVUTANO wa kisiasa na kijeshi nchini Uganda unaongezeka kufuatia hatua ya Mkuu wa Jeshi Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kuendelea kukamata maafisa wakuu wa jeshi na kutoa vitisho dhidi ya Makamu wa Rais Jessica Alupo.
Katika kipindi cha miezi 15 iliyopita majenerali na maafisa wakuu 12 wa kijeshi wamenaswa katika msako unaoongozwa na Kainerugaba, ambaye pia ni mwanawe Rais Museveni.
Kainerugaba mwenye umri wa miaka 52 anaonekana na wengi kuwa mmoja wa watu wanaoweza kumrithi babake, ingawa azma yake inaripotiwa kukumbwa na upinzani ndani ya chama tawala National Resistance Movement (NRM).
Katika kikao cha viongozi wakuu wa NRM mnamo Jumanne wiki iliyopita, hakukuwa na makubaliano kuhusu pendekezo la kumuunga mkono Kainerugaba amrithi Museveni.
Baadhi ya viongozi waliripotiwa kupinga mpango huo huku wengine wakitilia shaka uwezo wake wa kuongoza serikali ya kiraia.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa NRM Richard Todwong Awany alikanusha madai kwamba chama kimekataa kumuunga mkono Jenerali huyo, akisema maamuzi yoyote yatatangazwa rasmi kwa wakati unaofaa.
Jumatatu usiku ya Novemba 9 Kainerugaba alimtaka Makamu wa Rais Jessica Alupo kujiandaa kuondoka ofisini, akisema ni yeye ndiye anapaswa kuchukua nafasi hiyo.
“Yeyote aliye katika ofisi hiyo anapaswa kujiandaa kuikabidhi hivi karibuni,” aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani Twitter) kabla ya kufuta ujumbe huo.
Aidha, alitishia kumfukuza kazi Alupo na kumkamata iwapo uchunguzi ungeonyesha kuhusika kwake katika kile alichokiita…