📰 Newspapers

Mwalimu anayekuza vipaji kwa kalamu na sanaa

Mwalimu anayekuza vipaji kwa kalamu na sanaa

MWALIMU bora anapaswa kuwa na maarifa mapana yanayozidi yale ya wanafunzi wake, huku akiwa na ari ya kujifunza mambo mapya kila wakati.

Anapobaini kuwa wanafunzi wake wana ufahamu mkubwa kuliko yeye katika baadhi ya maeneo, anapaswa kujituma zaidi katika utafiti ili kupanua maarifa yake na kukidhi mahitaji ya darasa analoliongoza.

Kwa mtazamo wa Bw Mwangi wa Githinji, wanafunzi humwamini zaidi mwalimu mwenye ufahamu mpana wa somo analofundisha na anayefuatilia kwa karibu masuala yote yanayohusiana na mtaala.

“Sawa na dereva wa gari anayewajibika kuwafikisha abiria wao salama mwisho wa safari, mwalimu naye ana jukumu la kuwaongoza wanafunzi kwa nidhamu na utaalamu hadi watimize ndoto zao za kielimu,” anasema.

Mwangi alilelewa katika kijiji cha Karima, Othaya, Kaunti ya Nyeri. Ni mtoto wa pili katika familia ya watoto wanne ya Bw Bassilius Githinji na Bi Mary Wambui.

Alianza safari yake ya elimu katika Shule ya Msingi ya Karima (1995–2005), kabla ya kujiunga na Shule ya Upili ya Giakanja Boys, Nyeri (2006–2009).

Baadaye alijiunga na Chuo cha Mafunzo ya Walimu cha Tambach, Kaunti ya Elgeyo-Marakwet, ambako alisomea ualimu kati ya 2010 na 2012.

Mbali na Bw Maina Wanyiri, aliyempa msingi imara wa elimu katika shule ya msingi, Bi Wanjau, aliyemfundisha Kiswahili katika shule ya upili, alikuwa miongoni mwa watu waliomchochea kuchagua taaluma ya ualimu.

In brief

MWALIMU bora anapaswa kuwa na maarifa mapana yanayozidi yale ya wanafunzi wake, huku akiwa na ari ya kujifunza mambo mapya kila wakati. Anapobaini kuwa wanafunzi wake wana ufahamu mkubwa kuliko yeye katika baadhi ya maeneo, anapaswa kujituma zaidi katika utafiti ili kupanua maarifa yake na kukidhi mahitaji ya darasa analoliongoza. Mwangi alilelewa katika kijiji cha Karima, Othaya, Kaunti ya Nyeri.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.