📰 Newspapers

Wasiwasi waingia kuhusu nyumba nafuu kuwa bila hatimiliki

Wasiwasi waingia kuhusu nyumba nafuu kuwa bila hatimiliki

SERIKALI imeharakisha mchakato wa kupata hatimiliki za ardhi inayotumiwa kujenga nyumba za gharama nafuu, baada ya kubainika kuwa zaidi ya asilimia 90 ya ardhi iliyotengewa mpango huo haina stakabadhi za umiliki.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Nyumba za Gharama Nafuu Joe Mutugu, aliambia Kamati ya Bunge kuhusu Hesabu za Hazina Maalumu kuwa Baraza la Mawaziri limeidhinisha kuhamishwa kwa vipande 275 vya ardhi vinavyomilikiwa na serikali kuu kwa mpango huo.

Aidha, magavana katika kaunti ambako miradi inatekelezwa kwenye ardhi ya serikali za kaunti wametia saini makubaliano ya kuwezesha kutolewa kwa hatimiliki.

Serikali inatarajia barua nyingi kukamilika kufikia Disemba 2026.

“Serikali inafanya juhudi za kushughulikia hatimiliki ili kuhakikisha miradi yote inakuwa na umiliki salama wa ardhi,” akasema Bw Mutugu.

Mnamo Novemba 2025, Baraza la Magavana (COG) lilifichua kuwa ekari 486 kati ya 540 zilizokabidhiwa serikali kwa ajili ya miradi hiyo hazikuwa na hatimiliki.

Ripoti maalumu ya Mkaguzi Mkuu pia ilibaini kuwa miradi 269 kati ya iliyokaguliwa haikuwa na barua zozote za umiliki wa ardhi, hali iliyozua wasiwasi kuhusu usalama wa miradi hiyo kisheria.

Serikali inalenga kujenga nyumba 250,000 kila mwaka, huku zaidi ya nyumba 277,000 zikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi na 11,400 zikiwa zimekamilika.

Mpango huo unalenga makundi mbalimbali ya mapato, huku bei za nyumba zikiwa kati ya Sh840,000 na Sh5.76 milioni.

In brief

SERIKALI imeharakisha mchakato wa kupata hatimiliki za ardhi inayotumiwa kujenga nyumba za gharama nafuu, baada ya kubainika kuwa zaidi ya asilimia 90 ya ardhi iliyotengewa mpango huo haina stakabadhi za umiliki. Aidha, magavana katika kaunti ambako miradi inatekelezwa kwenye ardhi ya serikali za kaunti wametia saini makubaliano ya kuwezesha kutolewa kwa hatimiliki. “Serikali inafanya juhudi za kushughulikia hatimiliki ili kuhakikisha miradi yote inakuwa na umiliki salama wa ardhi,” akasema Bw Mutugu.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.