📰 Newspapers

Kurejea kwa Jumwa UDA kunavyobadili hali ya siasa Kilifi

Kurejea kwa Jumwa UDA kunavyobadili hali ya siasa Kilifi

SIASA za Kaunti ya Kilifi zinatarajiwa kuchukua mwelekeo mpya baada ya aliyekuwa Waziri wa Baraza la Mawaziri (CS) Aisha Jumwa kurejea katika chama tawala cha United Democratic Alliance (UDA), miezi minne baada ya kukihama kutokana na kutoridhishwa na jinsi chama hicho kilivyoshughulikia azma yake ya kuwania ugavana mwaka 2027.

Kurejea kwa Bi Jumwa kunatarajiwa kumkosesha usingizi Gavana wa sasa wa Kilifi Gideon Mung’aro, ambaye anatafuta kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili kupitia chama cha Orange Democratic Movement (ODM).

Hali hiyo inazidi kuchanganya hesabu za kisiasa katika kaunti hiyo, hasa wakati ambapo mipango ya vyama vya UDA na ODM kushirikiana katika kugawana nafasi za kisiasa kupitia mfumo wa ‘zoning’ inaonekana kukabiliwa na changamoto.

Iwapo Bi Jumwa ataendeleza azma yake ya kuwania ugavana na kupata uungwaji mkono wa viongozi na wanachama wa UDA pamoja na Pamoja African Alliance (PAA), huenda Bw Mung’aro akakabiliwa na ushindani mkali katika uchaguzi mkuu wa 2027.

Spika wa Seneti Amason Kingi, ambaye ni kiongozi wa PAA, awali alisema chama chake kitaunga mkono wagombeaji wa UDA katika nafasi zote za uchaguzi mkuu ujao, hatua inayoweza kuimarisha nafasi ya Bi Jumwa iwapo atapewa tiketi ya chama hicho.

Aidha, mmoja wa wanasiasa wenye ushawishi Kilifi, Bw George Kithi, ambaye kwa sasa anaunga mkono UDA, anaweza pia kuwa miongoni mwa viongozi watakaounga mkono azma ya Bi Jumwa.

In brief

SIASA za Kaunti ya Kilifi zinatarajiwa kuchukua mwelekeo mpya baada ya aliyekuwa Waziri wa Baraza la Mawaziri (CS) Aisha Jumwa kurejea katika chama tawala cha United Democratic Alliance (UDA), miezi minne baada ya kukihama kutokana na kutoridhishwa na jinsi chama hicho kilivyoshughulikia azma yake ya kuwania ugavana mwaka 2027. Spika wa Seneti Amason Kingi, ambaye ni kiongozi wa PAA, awali alisema chama chake kitaunga mkono wagombeaji wa UDA katika nafasi zote za uchaguzi mkuu ujao, hatua inayoweza kuimarisha nafasi ya Bi Jumwa iwapo atapewa tiketi ya chama hicho.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.