📰 Newspapers

Kinyang’anyiro cha mabilionea? Tathmini yaonyesha unahitaji karibu Sh20bn kampeni ya urais

Kinyang’anyiro cha mabilionea? Tathmini yaonyesha unahitaji karibu Sh20bn kampeni ya urais

WAGOMBEAJI wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027 wanakabiliwa na gharama kubwa za kuendesha kampeni za kitaifa, huku makadirio yakionyesha kuwa shughuli hizo zinaweza kugharimu kati ya Sh10 bilioni na Sh20 bilioni.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imeweka kiwango cha juu cha matumizi ya kampeni za urais kuwa Sh6.1 bilioni.

Hata hivyo, kiwango hicho kinahusu kipindi rasmi cha kampeni cha miezi miwili, ilhali wagombeaji wengi wameanza kujitangaza na kutafuta uungwaji mkono mapema.

Prof Karuti Kanyinga, mchanganuzi wa masuala ya kisiasa na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nairobi, anakadiria kuwa kampeni madhubuti za urais zinaweza kugharimu Sh14 bilioni.

Wagombeaji wanahitaji kufikia wapigakura katika kaunti zote 47 na maeneobunge 290 ya uchaguzi.

Haja ya kujenga mitandao ya kimataifa na kutafuta michango imewafanya baadhi ya viongozi wa upinzani kuelekea Amerika, ambako kuna idadi kubwa ya Wakenya wanaoishi ughaibuni.

Aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua alirejea nchini Oktoba 20 baada ya ziara ya siku 50 nchini Amerika, ambako alikutana na Wakenya na kuendesha shughuli za kuchangisha fedha.

Kiongozi wa Linda Mwananchi, Edwin Sifuna anapanga ziara ya wiki mbili kuanzia Novemba 20, huku Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka akiahirisha ziara yake nchini Amerika hadi Februari 2027.

Viongozi wengine, akiwemo Dkt Fred Matiang'i na Jimmy Wanjigi, wameajiri kampuni za Amerika kupiga jeki kampeni zao na kuimarisha mitandao ya kimataifa.

In brief

WAGOMBEAJI wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027 wanakabiliwa na gharama kubwa za kuendesha kampeni za kitaifa, huku makadirio yakionyesha kuwa shughuli hizo zinaweza kugharimu kati ya Sh10 bilioni na Sh20 bilioni. Prof Karuti Kanyinga, mchanganuzi wa masuala ya kisiasa na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nairobi, anakadiria kuwa kampeni madhubuti za urais zinaweza kugharimu Sh14 bilioni.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.