📰 Newspapers

Kenya yalenga historia dhidi ya Afrika Kusini leo dimba la kufuzu AFCON 2027

Kenya yalenga historia dhidi ya Afrika Kusini leo dimba la kufuzu AFCON 2027

TIMU ya taifa Harambee Stars itakuwa na nafasi nyingine ya kuandikisha historia itakapomenyana na Afrika Kusini katika mechi ya marudiano ya kufuzu kwa Kombe la Afrika (AFCON) 2027, uwanjani Nyayo, Nairobi, leo jioni.

Kenya itakuwa na hamu ya kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Bafana Bafana katika muda wa kawaida wa mchezo baada ya timu hizo kutoka sare ya kusisimua ya 2-2 mechi ya kwanza iliyochezewa mjini Soweto, Ijumaa iliyopita.

Stars walionyesha ukakamavu mkubwa kwa kurejea mchezoni mara mbili licha ya kujifunga kupitia Amos Wanjala dakika ya tisa.

Nahodha Michael Olunga alisawazisha kupitia penalti dakika ya 44.

Relebohile Mofokeng alirejesha Afrika Kusini uongozini dakika ya 77.

Lakini Ryan Ogam, aliyeingia kipindi cha pili, alinyamazisha mashabiki wa Soweto kwa kusawazisha dakika ya 89.

Kenya, ambayo tayari imefuzu moja kwa moja kwa AFCON 2027 kama mmoja wa mataifa wenyeji, ilivuruga mipango ya Afrika Kusini ya kutwaa nafasi pekee ya kufuzu katika Kundi D.

Stars wamepata nguvu zaidi baada ya beki Zak Vyner, anayesekatia Wrexham nchini Uingereza, kujiunga na kikosi hicho jijini Nairobi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa akiwa na Stars.

Vyner, ambaye anaweza kucheza kama difenda au kiungo mkabaji, anatarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya Kenya katika mechi hiyo muhimu.

In brief

TIMU ya taifa Harambee Stars itakuwa na nafasi nyingine ya kuandikisha historia itakapomenyana na Afrika Kusini katika mechi ya marudiano ya kufuzu kwa Kombe la Afrika (AFCON) 2027, uwanjani Nyayo, Nairobi, leo jioni. Relebohile Mofokeng alirejesha Afrika Kusini uongozini dakika ya 77. Kenya, ambayo tayari imefuzu moja kwa moja kwa AFCON 2027 kama mmoja wa mataifa wenyeji, ilivuruga mipango ya Afrika Kusini ya kutwaa nafasi pekee ya kufuzu katika Kundi D.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.