📰 Newspapers

MAONI: Huenda Babu Owino akabaki yatima wa kisiasa kwa kujipambania kivyake

MAONI: Huenda Babu Owino akabaki yatima wa kisiasa kwa kujipambania kivyake

UCHAGUZI wa ugavana wa Nairobi wa mwaka ujao unazidi kuwa mtihani mgumu wa kisiasa kwa Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino.

Awali alichukuliwa kama mmoja wa wagombea wenye nafasi kubwa ya kutwaa usukani wa Jiji la Nairobi ila Babu sasa amejikuta katika mazingira magumu ya kisiasa yanayotawaliwa na ushindani wa madaraka, mazungumzo ya miungano na kutokuwa na uhakika kuhusu nani anayedhibiti mwelekeo wa upinzani.

Kiini cha dhoruba hii ni ushindani unaochipuka kati ya azma ya Babu ya kuwania ugavana na hesabu pana za kisiasa za Muungano wa Upinzani.

Chama cha DCP, chini ya uongozi wa Rigathi Gachagua, kimeonekana kumpa James Gakuya nafasi ya kuwa mgombea wake wa ugavana wa Nairobi.

Hali hii inamweka Babu katika mazingira magumu, hasa iwapo upinzani utaamua kuwa na mgombea mmoja wa pamoja.

Hali inazidi kuwa tata kutokana na kuingia kwa kundi la Linda Mwananchi linalohusishwa na Seneta Edwin Sifuna.

Babu ni miongoni mwa watu waliokuwa na mchango mkubwa katika kuanzishwa kwa vuguvugu la Linda Mwananchi kabla ya kusajili chama cha The Mwananchi Party (TMP) kama chombo chake cha kisiasa.

Suala hili linampaka tope machoni pa wenzake kuwa mwanasiasa mnafiki anayetanguliza malengo yake bila kuwahusisha wenzake.

Ikiwa Sifuna alikuwa na imani na chama kipya chake Babu Owino - TMP, asingeendelea na mpango wa kukisajili chama cha Linda Mwananchi Movement.

In brief

UCHAGUZI wa ugavana wa Nairobi wa mwaka ujao unazidi kuwa mtihani mgumu wa kisiasa kwa Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino. Hali hii inamweka Babu katika mazingira magumu, hasa iwapo upinzani utaamua kuwa na mgombea mmoja wa pamoja. Ikiwa Sifuna alikuwa na imani na chama kipya chake Babu Owino - TMP, asingeendelea na mpango wa kukisajili chama cha Linda Mwananchi Movement.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.