📰 Newspapers

Rais Ruto kwenye mizani akihutubia Bunge kuhusu hali ya taifa Alhamisi

Rais Ruto kwenye mizani akihutubia Bunge kuhusu hali ya taifa Alhamisi

RAIS William Ruto anatarajiwa kutoa hotuba yake ya nne kuhusu hali ya taifa kesho mbele ya kikao cha pamoja cha Bunge la Kitaifa na Seneti, huku serikali yake ikikabiliwa na changamoto za deni la taifa, gharama ya maisha na ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana.

Hotuba hiyo inajiri siku chache baada ya Ofisi ya Bajeti ya Bunge (PBO) kuonya kuwa serikali ina nafasi finyu ya kifedha kutekeleza mipango yake kutokana na mzigo mkubwa wa madeni.

Ripoti ya PBO kuhusu chaguo za bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2027/28 inaonyesha kuwa bajeti ya kawaida inatarajiwa kuwa Sh5.3 trilioni, huku Sh1.5 trilioni zikitumika kulipa riba ya madeni pekee. Kiasi hicho ni zaidi ya mara mbili ya fedha zinazotengewa miradi ya maendeleo.

Deni la taifa limefikia Sh13.1 trilioni, huku serikali ikirekodi upungufu wa mapato wa Sh60.2 bilioni kufikia Juni 2026.

Hotuba hiyo pia inatolewa miezi minane kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 2027, hivyo Rais Ruto anatarajiwa kueleza mafanikio ya serikali yake na kutoa majibu kuhusu changamoto zinazowakabili wananchi.

Mtaalamu wa utawala Barasa Nyukuri, anasema hotuba hiyo itakuwa kipimo cha utendaji wa serikali, hasa ikilinganishwa na ahadi zake za kiuchumi na miradi mikubwa.

Anasema Rais anapaswa kueleza jinsi atakavyokabiliana na ukosefu wa ajira kwa vijana, ufadhili wa vyuo vikuu, maandalizi ya uchaguzi, deni la taifa na gharama ya maisha.

In brief

RAIS William Ruto anatarajiwa kutoa hotuba yake ya nne kuhusu hali ya taifa kesho mbele ya kikao cha pamoja cha Bunge la Kitaifa na Seneti, huku serikali yake ikikabiliwa na changamoto za deni la taifa, gharama ya maisha na ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana. Hotuba hiyo pia inatolewa miezi minane kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 2027, hivyo Rais Ruto anatarajiwa kueleza mafanikio ya serikali yake na kutoa majibu kuhusu changamoto zinazowakabili wananchi.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.