📰 Newspapers

Afisa wa Gavana Natembeya aendelea kuuguza majeraha mabaya baada ya kushambuliwa

Afisa wa Gavana Natembeya aendelea kuuguza majeraha mabaya baada ya kushambuliwa

AFISA wa mawasiliano wa Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, Amos Boaz Masika, maarufu kama Hammer Hammer Ke, amelazwa hospitalini Eldoret baada ya kushambuliwa kwa mapanga na watu wenye silaha karibu na nyumbani kwake.

Bw Masika alijeruhiwa vibaya kichwani, mikononi na miguuni katika tukio lililotokea Jumatatu, Novemba 16, mwendo wa saa mbili na nusu usiku, eneo la Chebarus. Washambuliaji pia walichoma gari lake.

Wakati wa shambulizi hilo, alikuwa akirejea nyumbani akiwa na bintiye mdogo. Mtoto huyo aliokolewa na kupelekwa na mamake mahali salama.

Nduguye, Bw Sam Masika, alisema familia imeshtushwa na ukatili huo na kuwataka polisi kuwakamata wahusika.

“Jinsi alivyoshambuliwa inaonyesha washambuliaji walikuwa na nia ya kumuua. Ninataka polisi wawasake na kuwakamata,” alisema.

Tukio hilo limezua ghadhabu miongoni mwa viongozi, wanablogu na watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa chama cha Linda Mwananchi Pauline Njoroge, alilaani shambulizi hilo, akilihusisha na mazingira ya hofu kwa wanaotoa maoni ya kisiasa.

Hata hivyo, hakuna ushahidi uliowasilishwa kuthibitisha uhusiano huo.

Mnamo Oktoba 22 Masika alikamatwa karibu na Mahakama ya Kitale na baadaye kushtakiwa kwa unyanyasaji wa mtandaoni.

Polisi wamesema uchunguzi kuhusu shambulizi hilo unaendelea kubaini waliohusika na nia yao.

In brief

AFISA wa mawasiliano wa Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, Amos Boaz Masika, maarufu kama Hammer Hammer Ke, amelazwa hospitalini Eldoret baada ya kushambuliwa kwa mapanga na watu wenye silaha karibu na nyumbani kwake. Wakati wa shambulizi hilo, alikuwa akirejea nyumbani akiwa na bintiye mdogo. Polisi wamesema uchunguzi kuhusu shambulizi hilo unaendelea kubaini waliohusika na nia yao.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.