📰 Newspapers

Kutana na mwanamke fundi wa magari anayetambulika kimataifa

Kutana na mwanamke fundi wa magari anayetambulika kimataifa

KWA miaka mingi, umekanika umekuwa ukichukuliwa kuwa kazi ya wanaume. Lakini Martha Njeri Wambui anathibitisha kuwa hakuna suala la jinsia ikija kwa ujuzi, bidii na kujiamini.

Leo, mwanamke huyo si fundi wa kawaida katika kampuni ya Isuzu East Africa.

Ameandika historia kwa kupata nafasi ya kuiwakilisha kampuni hiyo katika mashindano ya kimataifa ya Isuzu Grand Prix nchini Japan, ambako mekanika kutoka takriban nchi 34 hukutana kuonyesha umahiri wao.

Safari yake haikuwa ya bahati. Ilianza mwaka 2014 alipojiunga na Chuo cha Ufundi cha Kabete kusomea uhandisi wa mitambo.

Ingawa hakuwahi kuota kuwa fundi wa magari alipokuwa mtoto, shauku ya binamu yake kuhusu mifumo ya nyaya za magari na taaluma ya mjomba wake katika uhandisi wa mitambo ilimvutia.

Baada ya kuhitimu mwaka 2018, Njeri alijitosa katika ulimwengu wa kazi kupitia mafunzo ya vitendo katika Ruaka Auto Garage, Marshalls, KVM na Farmer’s Choice.

Mwaka 2021, maisha yake yalipata mwelekeo mpya alipojiunga na mpango wa Isuzu East Africa wa Indentured Learners Programme, uliolenga kuwapa wahitimu ujuzi unaohitajika katika sekta ya magari.

Baadaye alifanya kazi katika kitengo cha kuunganisha magari kwa miaka miwili kabla ya kuhamia idara ya huduma za baada ya mauzo kama fundi.

Uwezo wake ulidhihirika katika mashindano ya Isuzu Grand Prix, ambapo alishika nafasi ya tatu kati ya washiriki takriban 12 katika kundi lake na kuwa mwanamke bora zaidi.

In brief

KWA miaka mingi, umekanika umekuwa ukichukuliwa kuwa kazi ya wanaume. Leo, mwanamke huyo si fundi wa kawaida katika kampuni ya Isuzu East Africa. Ingawa hakuwahi kuota kuwa fundi wa magari alipokuwa mtoto, shauku ya binamu yake kuhusu mifumo ya nyaya za magari na taaluma ya mjomba wake katika uhandisi wa mitambo ilimvutia. Uwezo wake ulidhihirika katika mashindano ya Isuzu Grand Prix, ambapo alishika nafasi ya tatu kati ya washiriki takriban 12 katika kundi lake na kuwa mwanamke bora zaidi.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.