📰 Newspapers

Taharuki kiongozi wa upinzani akishtakiwa

Taharuki kiongozi wa upinzani akishtakiwa

MAPUTO, Msumbiji: KIONGOZI wa upinzani nchini Msumbiji, Venancio Mondlane, Jumanne alifikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka ya kuchochea ugaidi na uasi kuhusiana na machafuko yaliyosababisha vifo vya watu baada ya uchaguzi wa 2024 uliokumbwa na utata. Mondlane amekanusha mashtaka yote dhidi yake, akisema kesi hiyo ina nia ya kisiasa na inalenga kumwadhibu kwa msimamo wake dhidi ya serikali. Zaidi ya watu 300…

MAPUTO, Msumbiji:

KIONGOZI wa upinzani nchini Msumbiji, Venancio Mondlane, Jumanne alifikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka ya kuchochea ugaidi na uasi kuhusiana na machafuko yaliyosababisha vifo vya watu baada ya uchaguzi wa 2024 uliokumbwa na utata.

Mondlane amekanusha mashtaka yote dhidi yake, akisema kesi hiyo ina nia ya kisiasa na inalenga kumwadhibu kwa msimamo wake dhidi ya serikali.

Zaidi ya watu 300 waliuawa katika maandamano yaliyofuatia uchaguzi huo, kulingana na kundi la mashirika ya kiraia yanayofuatilia matukio nchini.

Maandamano hayo yalikuwa makubwa zaidi kuwahi kufanyika dhidi ya chama tawala cha Frelimo, ambacho kimekuwa madarakani tangu Msumbiji ipate uhuru mnamo 1975.

Upinzani unadai kuwa Rais Daniel Chapo na Frelimo walishinda uchaguzi kupitia wizi wa kura, madai ambayo rais na chama chake wamekanusha.

Waangalizi wa uchaguzi kutoka mataifa ya Magharibi walisema wakati huo kuwa uchaguzi huo haukuwa huru wala wa haki.

Polisi na magari yao yalitumwa Jumanne katika barabara zote zinazoelekea Mahakama ya Juu, ambako kesi ya Mondlane ilianza.

Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kwa miezi kadhaa.

Maelfu ya wafuasi wa Mondlane walikusanyika nje ya mahakama, wakilitaja jina lake kwa shangwe na kumpungia mikono alipojitokeza.

Mondlane aliwaambia waandishi wa habari kuwa alikuwa mtulivu na mwenye matumaini kutokana na maandalizi yaliyofanywa na mawakili wake.

Mahakama imepiga marufuku matangazo ya moja kwa moja ya kesi hiyo, ikisema hatua hiyo inalenga kuzuia uwezekano wa machafuko na kuvurugika…

In brief

MAPUTO, Msumbiji: KIONGOZI wa upinzani nchini Msumbiji, Venancio Mondlane, Jumanne alifikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka ya kuchochea ugaidi na uasi kuhusiana na machafuko yaliyosababisha vifo vya watu baada ya uchaguzi wa 2024 uliokumbwa na utata. Mondlane amekanusha mashtaka yote dhidi yake, akisema kesi hiyo ina nia ya kisiasa na inalenga kumwadhibu kwa msimamo wake dhidi ya serikali.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.