MISIMAMO mikali miongoni mwa wandani wa Kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka na Edwin Sifuna wa Linda Mwananchi inatishia kutatiza juhudi za upinzani kuwa na mwaniaji mmoja wa urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Licha ya viongozi hao wawili kuahidi kuunga mkono juhudi za ushirikiano kumkabili Rais William Ruto, wandani wao wanazidi kusukuma mbele azma zao za urais, kila upande ukisisitiza kuwa kiongozi wao ndiye mwenye nafasi nzuri ya kushinda.
Washirika wa Bw Sifuna wanadai umaarufu wake unaoongezeka, hasa Magharibi mwa Kenya na miongoni mwa vijana, unamfanya kuwa mgombea anayefaa kupewa tiketi ya upinzani.
Hata hivyo, wandani wa Bw Musyoka nao wanasisitiza kuwa uzoefu wake wa kisiasa na tajriba yake ya uongozi, inampa nafasi bora ya kuongoza upinzani.
Mzozo huo pia umefichua mgawanyiko Magharibi mwa Kenya kuhusu ni nani anayefaa kuwakilisha eneo hilo katika mazungumzo ya kuunda muungano, huku washirika wa Bw Sifuna wakitilia shaka nafasi ya kiongozi wa DAP-Kenya Eugene Wamalwa.
Katika kongamano la kitaifa la wajumbe wa Linda Mwananchi lililofanyika wiki iliyopita, wajumbe walimpa Bw Sifuna mamlaka ya kuongoza mazungumzo na vyama vinavyoshikilia msimamo kama wao kabla ya uchaguzi.
Hata hivyo, washirika wake wanasisitiza kuwa mazungumzo hayo yanapaswa kuzingatia azma yake ya kuwania urais.
Seneta wa Kakamega, Boni Khalwale aliambia Taifa Leo kuwa viongozi wa upinzani wanapaswa kuzingatia umaarufu wa Bw Sifuna wanapochagua mgombea wao, akisema atazungumza kwa niaba ya…