📰 Newspapers

Sifuna, washirika wasusia hotuba ya Ruto wakilalamikia ukiukaji wa haki za kimsingi

Sifuna, washirika wasusia hotuba ya Ruto wakilalamikia ukiukaji wa haki za kimsingi

KIONGOZI wa Linda Mwananchi Movement (LMM) Edwin Sifuna na washirika wake katika upinzani walisusia hotuba ya Hali ya Taifa ya Rais William Ruto bungeni, wakipinga visa vya utekaji nyara na vitisho dhidi ya wakosoaji wa serikali.

Badala yake, walizindua rasmi mrengo wa wanawake wa chama hicho, ‘Dada za Sifuna’, katika makao makuu ya chama jijini Nairobi, hafla iliyohudhuriwa na viongozi kadhaa.

Sifuna, ambaye pia ni Seneta wa Nairobi, alisema aliamua kususia kikao hicho kwa sababu kanuni za Bunge zinamtaka Rais asikilizwe kwa utulivu, hata anapotoa madai ambayo upinzani haukubaliani nayo.

“Rais anaenda bungeni kudanganya tena. Kanuni za Bunge zinamtaka Rais asikilizwe kwa utulivu. Baadhi yetu hatuwezi kukaa kimya bila kumwambia kuwa anadanganya,” alisema.

Alisema hotuba hiyo inapaswa kueleza hali halisi ya wananchi, uchumi na usalama nchini, badala ya Rais kujikita katika kutaja miradi ya maendeleo.

Sifuna alirejelea Kifungu cha 132 cha Katiba kinachomtaka Rais kutoa hotuba kwa taifa kila mwaka kuhusu hatua zilizochukuliwa na maendeleo yaliyopatikana katika kutekeleza maadili ya kitaifa inavyofafanuliwa katika Kifungu cha 10.

Alisema maadili hayo yanahusu haki za binadamu, demokrasia, utawala wa sheria, uhuru, ushirikishaji na haki, akidai visa vya utekaji nyara bado vinaripotiwa chini ya utawala wa Rais Ruto.

LMM pia ilieleza wasiwasi kuhusu mashambulizi dhidi ya watu wanaotetea demokrasia, ikiwemo shambulizi la hivi karibuni dhidi ya Amos Boaz Masika, mfanyakazi katika Trans Nzoia.

In brief

KIONGOZI wa Linda Mwananchi Movement (LMM) Edwin Sifuna na washirika wake katika upinzani walisusia hotuba ya Hali ya Taifa ya Rais William Ruto bungeni, wakipinga visa vya utekaji nyara na vitisho dhidi ya wakosoaji wa serikali. Kanuni za Bunge zinamtaka Rais asikilizwe kwa utulivu. Alisema hotuba hiyo inapaswa kueleza hali halisi ya wananchi, uchumi na usalama nchini, badala ya Rais kujikita katika kutaja miradi ya maendeleo.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.