📰 Newspapers

Polisi waokoa mtoto ‘aliyeuzwa’ kwa Sh150, 000

Polisi waokoa mtoto ‘aliyeuzwa’ kwa Sh150, 000

POLISI wamefanikiwa kumuokoa msichana wa miaka minne aliyetekwa nyara akicheza na watoto wengine katika uwanja wa wazi karibu na nyumbani kwao Malaa, Kaunti ya Machakos na kudaiwa kuuzwa kwa Sh150,000.

Maafisa pia wamewakamata washukiwa wanne katika operesheni zilizofanyika Utawala, Nairobi na Meru kuhusiana na utekaji huo.

Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), mwanamke aliyekuwa amejifunika kichwa kwa hijab alimshawishi mtoto huyo kuandamana naye kwa kisingizio cha kumpeleka dukani kununua sukari na chokoleti.

Mama wa mtoto alipofika kumchukua, watoto wenzake walimweleza kuwa mwanamke huyo alikuwa amemchukua.

Uchunguzi uliwawezesha wapelelezi kumkamata mshukiwa wa kwanza eneo la Tutua, kaunti ya Meru, kabla ya wengine watatu kunaswa Utawala karibu na duka la Quickmart.

Kamanda wa Polisi wa Matungulu Peter Gichohi, alisema mtoto alipatikana akiwa katika hali nzuri na kupelekwa Kituo cha Afya cha Nguluni kufanyiwa uchunguzi kabla ya kuunganishwa na wazazi wake.

Polisi wanachunguza madai kuwa mtoto huyo alikuwa ameuzwa kwa Sh150,000. Magari na pikipiki zinazoshukiwa kutumiwa katika uhalifu huo pia zilikamatwa.

In brief

POLISI wamefanikiwa kumuokoa msichana wa miaka minne aliyetekwa nyara akicheza na watoto wengine katika uwanja wa wazi karibu na nyumbani kwao Malaa, Kaunti ya Machakos na kudaiwa kuuzwa kwa Sh150,000. Mama wa mtoto alipofika kumchukua, watoto wenzake walimweleza kuwa mwanamke huyo alikuwa amemchukua. Kamanda wa Polisi wa Matungulu Peter Gichohi, alisema mtoto alipatikana akiwa katika hali nzuri na kupelekwa Kituo cha Afya cha Nguluni kufanyiwa uchunguzi kabla ya kuunganishwa na wazazi wake. Polisi wanachunguza madai kuwa mtoto huyo alikuwa ameuzwa kwa Sh150,000.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.