MDHIBITI wa Bajeti (CoB) Margaret Nyakang’o, amezua wasiwasi kuhusu hatua ya Kaunti ya Nairobi kukopa Sh1.5 bilioni kila mwezi kutoka Sidian Bank kulipa mishahara, licha ya serikali kuu kutoa mgao wa fedha kwa wakati.
Ripoti iliyowasilishwa mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, inaonyesha kuwa kaunti hiyo ilikopa Sh1.56 bilioni Septemba na Sh1.49 bilioni Oktoba.
Katika barua ya Novemba 16, 2026, Waziri wa Fedha wa Kaunti ya Nairobi Ibrahim Nyangoya Auma alithibitisha kuwa serikali ya kaunti ilitia saini makubaliano na Sidian Bank kuwezesha malipo ya mishahara.
Hata hivyo, baadhi ya makato ya wafanyakazi yaliyopaswa kupelekwa kwa vyama vya akiba na mikopo (SACCO), hazina za pensheni na taasisi nyingine hayakulipwa kikamilifu.
Benki hiyo ilionyesha kuwa Sh249.3 milioni za makato hayo Agosti bado hazijalipwa Septemba sawa na Sh254.5 milioni za Septemba zilizopaswa kulipwa Oktoba.
Katika barua ya Novemba 16, 2026, Waziri wa Fedha wa Kaunti ya Nairobi Ibrahim Nyangoya Auma alithibitisha kuwa serikali ya kaunti ilitia saini makubaliano na Sidian Bank kuwezesha malipo ya mishahara.
Alisema mpango huo ulilenga kushughulikia changamoto za haraka za kulipa wafanyakazi huku kaunti ikiimarisha mapato na usimamizi wa fedha.
Hata hivyo, Nyakang’o alihoji sababu ya kaunti kukopa ilhali mgao wa fedha kutoka Serikali ya Kitaifa haukuwa umechelewa.
“Hadi Oktoba, kaunti zilikuwa zimepokea mgao wao.



