📰 Newspapers

Upinzani waanza kujaribu kupenya ngome za Ruto

Upinzani waanza kujaribu kupenya ngome za Ruto

UPINZANI umeanza kupeleka kampeni zake katika maeneo yanayochukuliwa kuwa ngome za Rais William Ruto, huku viongozi wake wakijaribu kuunda muungano imara wa kumkabili katika uchaguzi mkuu wa 2027.

Hata hivyo, licha ya kuahidi kuungana na kumuunga mkono mgombea mmoja wa urais ili kuepuka kugawanya kura, viongozi hao bado wanakabiliwa na mvutano kuhusu nani atakayepeperusha tiketi hiyo na nafasi ya vyama vidogo katika muungano unaochipuka.

Mnamo Jumatano, kiongozi wa Wiper Patriotic Front (WPF) Kalonzo Musyoka, alipeleka kampeni zake Eldoret, ambako alimtangaza Dkt Ruto kuwa rais wa muhula mmoja na kusema hana nia ya kujiunga na serikali yake.

Bw Musyoka ambaye ni naibu rais wa zamani, aliwahakikishia wafuasi wake kuwa atasalia katika kambi ya upinzani licha ya kile alichokitaja kuwa juhudi za kumpa majina ya kisiasa na wapinzani wake.

“Amekuwa akiniita Bw 40, na kwa kweli yeye ni mdogo wangu kisiasa. Hilo pekee haliwezi kunifanya niondoke katika upinzani na kujiunga na kambi yake,” alisema Bw Musyoka, ambaye pia anaongoza muungano wa Ukombozi Alliance.

Alisema ni haki ya Wakenya kuamua iwapo watampa Rais Ruto muhula wa pili au watataka kiongozi mwingine mwaka ujao.

Alikosoa hotuba ya Rais kuhusu hali ya taifa, akisema haikushughulikia ipasavyo changamoto zinazowakabili wananchi, zikiwemo gharama ya maisha, ukosefu wa ajira na ukiukaji wa haki za binadamu.

In brief

UPINZANI umeanza kupeleka kampeni zake katika maeneo yanayochukuliwa kuwa ngome za Rais William Ruto, huku viongozi wake wakijaribu kuunda muungano imara wa kumkabili katika uchaguzi mkuu wa 2027. Bw Musyoka ambaye ni naibu rais wa zamani, aliwahakikishia wafuasi wake kuwa atasalia katika kambi ya upinzani licha ya kile alichokitaja kuwa juhudi za kumpa majina ya kisiasa na wapinzani wake.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.