📰 Newspapers

Ruto apeleka injili ya ‘Usawa’ magharibi akiahidi miradi ya mabilioni ya pesa

Ruto apeleka injili ya ‘Usawa’ magharibi akiahidi miradi ya mabilioni ya pesa

RAIS William Ruto ameahidi kutumia Sh15 bilioni kujenga kilomita 150 za barabara katika Kaunti ya Busia, huku akizindua miradi ya miundombinu na kutangaza mipango ya kuimarisha usalama na usambazaji wa umeme katika eneo hilo.

Dkt Ruto, aliyeanza ziara ya siku nne katika eneo la Magharibi mwa Kenya Alhamisi, pia aliahidi kuunganisha familia 16,000 na umeme katika Busia ndani ya miezi sita ijayo.

Katika ziara hiyo, aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa kambi ya Kikosi cha kukabiliana na fujo (GSU) eneo la Akichelesit, Teso Kaskazini, na kutangaza kuwa serikali itatenga Sh100 milioni kujenga nyumba za maafisa watakaohudumu hapo.

Alisema mradi huo utaimarisha usalama katika eneo hilo na kuhakikisha maafisa wa polisi wanapata mazingira bora ya kuishi wanapotekeleza wajibu wao wa kulinda wananchi na mali yao.

Rais pia alifungua Kituo cha Utamaduni cha Kakapel Iteso, kinacholenga kuhifadhi na kukuza urithi wa jamii ya Iteso.

Katika Kaunti ya Bungoma, alizindua Barabara ya Matisi-Bokoli-Milani-Teremi, akaweka jiwe la msingi la soko la Bokoli na kufungua Barabara ya Mfupi-Mukuyuni-Naitiri pamoja na soko la Naitiri.

Baada ya kutangaza miradi hiyo, Dkt Ruto alitumia ziara hiyo kuwataka wapinzani wake kukubali kupimwa na wapigakura kwa rekodi zao za maendeleo badala ya kutumia idadi ya watu wa jamii zao kujipatia nafasi za kisiasa.

Akiwahutubia wakazi wa Teso Kaskazini, alisema uchaguzi unapaswa kuwa kipimo cha kile viongozi wamefanyia wananchi, wala…

In brief

RAIS William Ruto ameahidi kutumia Sh15 bilioni kujenga kilomita 150 za barabara katika Kaunti ya Busia, huku akizindua miradi ya miundombinu na kutangaza mipango ya kuimarisha usalama na usambazaji wa umeme katika eneo hilo. Dkt Ruto, aliyeanza ziara ya siku nne katika eneo la Magharibi mwa Kenya Alhamisi, pia aliahidi kuunganisha familia 16,000 na umeme katika Busia ndani ya miezi sita ijayo.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.