📰 Newspapers

Uraibu wa uvutaji sigara na shisha unavyochangia madhara ya muda mrefu

Uraibu wa uvutaji sigara na shisha unavyochangia madhara ya muda mrefu

MWENDO wa saa sita usiku mnamo Julai mwaka huu, Mzee Jay Mwashe*, 77 akiwa usingizini, alihisi maumivu fulani kifuani.

Lakini muda mfupi baadaye, alihisi kana kwamba anataka kukohoa, kabla ya kuanza kutatizika kupumua.

Tukio hilo lilibadilika mara moja na kuwa suala la dharura ambapo juhudi zilifanywa na akafikishwa hospitalini ambapo aliwekwa kwenye oksijeni mara moja kumsaidia kupumua.

Baada ya ukaguzi alibainika kuwa na tatizo la moyo lililochangiwa na Ugonjwa Sugu wa Kuziba Mapafu (Chronic Obstructive Pulmonary Disease (COPD).

Daktari alimfafanulia kuwa mojawapo ya masuala yanayochangia hali hiyo ni uvutaji sigara licha ya kuwa aliacha kuzivuta takriban miaka 30 iliyopita.

“Mimi niliacha kuvuta sigara karibu miaka 30 iliyopita, itakuwaje sasa nielezwe ndio jambo linalochangia hali ninayoshuhudia sasa?” aliuliza huku akijipata hospitali mara kadha baada ya hapo akilazimika kuwekwa kwenye oksijeni.

Ingawa mzee huyu sasa anaendelea na matibabu ambayo ni pamoja na kutumia kivuta pumzi(inhaler) kama watu wanaougua pumu, wataalam, wanasema hilo si jambo geni kwani uvutaji sigara una athari za muda mrefu kwa wanaozivuta na hata wale waliopo karibu na mazingira ya watu wanaozivuta.

Kulingana na Dkt Joseph Aluoch, tabibu na mtaalam wa kifua, madhara ya muda mrefu ya uvutaji sigara huathiri viungo muhimu vya mwili.

“Kuna madhara ya saratani ya mapafu, matatizo ya moyo, mshtuko wa moyo, ugonjwa sugu wa mkamba (bronchitis) miongoni ya mengine,” anaeleza.

In brief

MWENDO wa saa sita usiku mnamo Julai mwaka huu, Mzee Jay Mwashe*, 77 akiwa usingizini, alihisi maumivu fulani kifuani. Daktari alimfafanulia kuwa mojawapo ya masuala yanayochangia hali hiyo ni uvutaji sigara licha ya kuwa aliacha kuzivuta takriban miaka 30 iliyopita. “Mimi niliacha kuvuta sigara karibu miaka 30 iliyopita, itakuwaje sasa nielezwe ndio jambo linalochangia hali ninayoshuhudia sasa?” aliuliza huku akijipata hospitali mara kadha baada ya hapo akilazimika kuwekwa kwenye oksijeni.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.