📰 Newspapers

Tutatengeneza timu yetu vizuuuuri, asema Pochettino akianza kazi Man United

Tutatengeneza timu yetu vizuuuuri, asema Pochettino akianza kazi Man United

MAURICIO Pochettino jana alianza rasmi majukumu yake kama kocha mpya wa Manchester United baada ya kuwasili katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa Carrington.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 54 alisema ni heshima na fursa kubwa kuiongoza timu hiyo maarufu ya Uingereza.

Pochettino aliondoka kambini mwa timu ya taifa ya Amerika Jumanne usiku baada ya kuiongoza kulaza Haiti 2-0 mchana huo, katika mechi ya marudiano ya robo-fainali ya Ligi ya Mataifa ya Amerika Kaskazini na Kati na Caribbean (CONCACAF Nations League).

Alisafiri moja kwa moja hadi Manchester kuanza maandalizi ya kuinoa United, ambayo imempa mkataba wa miaka miwili na nusu baada ya kumruhusu kukamilisha majukumu yake ya kimataifa.

“Nina hamu kubwa kuanza kazi hapa. Ni heshima na fursa ya kipekee kuwa katika klabu hii kubwa. Natarajia kuanza kazi vizuri,” alisema Pochettino baada ya kuwasili uga wa mazoezi wa Carrington, Jumatano.

Kibarua chake cha kwanza ni mechi ngumu dhidi ya Liverpool katika Ligi Kuu Uingereza (EPL) hapo Jumapili.

Baada ya hapo watasafiri kuelekea nchini Ureno wiki ijayo kucheza dhidi ya Sporting Lisbon katika mchuano wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Hana muda mwingi wa kuzoea mazingira yake mapya ya kazi kwani wachezaji waliokuwa wakiwajibikia timu zao za taifa walirejea kambini jana.

Pochettino aliagana na Amerika kwa ujumbe wa kuatua moyo, akisema anajivunia mafanikio ambayo walipata kipindi akiwa usukani.

In brief

MAURICIO Pochettino jana alianza rasmi majukumu yake kama kocha mpya wa Manchester United baada ya kuwasili katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa Carrington. “Nina hamu kubwa kuanza kazi hapa. Ni heshima na fursa ya kipekee kuwa katika klabu hii kubwa. Natarajia kuanza kazi vizuri,” alisema Pochettino baada ya kuwasili uga wa mazoezi wa Carrington, Jumatano.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.