📰 Newspapers

Sh1.2 bilioni zimetumika kufidia waathiriwa wa maandamano

Sh1.2 bilioni zimetumika kufidia waathiriwa wa maandamano

JOPO la wataalamu wanaoshughulikia fidia kwa waathiriwa wa maandamano limeshughulikia maombi 1,476 na kulipa zaidi ya Sh1.218 bilioni, huku mwenyekiti Profesa Makau Mutua akitetea uadilifu wa zoezi hilo dhidi ya madai ya hongo.

Fidia hiyo ni kwa familia za waliouawa, waliojeruhiwa, manusura wa dhuluma za kingono na waliopata hasara za kiuchumi wakati wa maandamano na ukiukaji wa haki za binadamu tangu 2013.

Kiongozi wa kiufundi wa jopo hilo Richard Barno alisema walionufaika ni pamoja na familia za watu 236 waliouawa, 14 waliojeruhiwa vibaya sana, 214 waliojeruhiwa vibaya, 459 waliopata majeraha wastani na 369 waliopata majeraha madogo.

Wengine 14 walikuwa waathiriwa wa dhuluma za kingono, huku madai 170 yakihusu hasara za kiuchumi.

Barno alisema jopo hilo bado linachunguza zaidi ya faili 3,000 zilizowasilishwa kupitia ofisi zake na njia nyingine rasmi.

Mwanachama wa jopo hilo Dkt Duncan Ndeda alisema kiwango cha fidia hutegemea ukubwa wa majeraha na mazingira ya ukiukaji wa haki.

Waathiriwa wenye majeraha madogo hupokea Sh50,000, huku walio na majeraha ya wastani wakifidiwa Sh500,000.

Waliojeruhiwa vibaya hupata Sh1 milioni nao waliojeruhiwa vibaya sana wakilipwa kati ya Sh1.5 milioni na Sh3 milioni.

Familia za waliouawa hupokea angalau Sh3 milioni.

Ndeda alisema jopo linatumia njia mbadala kuthibitisha maombi ya waathiriwa ambao hawana ripoti za hospitali, hasa kutokana kuwa baadhi ya matukio yalitokea miaka mingi iliyopita.

In brief

JOPO la wataalamu wanaoshughulikia fidia kwa waathiriwa wa maandamano limeshughulikia maombi 1,476 na kulipa zaidi ya Sh1.218 bilioni, huku mwenyekiti Profesa Makau Mutua akitetea uadilifu wa zoezi hilo dhidi ya madai ya hongo. Kiongozi wa kiufundi wa jopo hilo Richard Barno alisema walionufaika ni pamoja na familia za watu 236 waliouawa, 14 waliojeruhiwa vibaya sana, 214 waliojeruhiwa vibaya, 459 waliopata majeraha wastani na 369 waliopata majeraha madogo.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.