📰 Newspapers

Sifuna asubiriwa kwa hamu Amerika ziara ya Kalonzo ikiahirishwa

Sifuna asubiriwa kwa hamu Amerika ziara ya Kalonzo ikiahirishwa

WAKENYA wanaoishi Amerika wanatazamia kwa hamu ziara ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, ambaye anatarajiwa kuwasili nchini humo huku akijipanga kuimarisha uungwaji mkono wake kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.

Ziara hiyo inatarajiwa kumwezesha Sifuna kukutana na Wakenya wanaoishi ughaibuni, kujadili uongozi wa Kenya na kutafuta michango ya kifedha kwa safari yake ya kisiasa.

Ziara hiyo inaanzia New Jersey na inaangazia umuhimu unaoongezeka wa wapiga kura na wafadhili waishio nje ya nchi katika siasa za Kenya.

Mwanzilishi mwenza wa The Equitable Party, Dkt Eunice Juma, alisema chama hicho kilikumbana na changamoto nyingi za kiutawala kikitafuta usajili.

“Wakati mwingine ilionekana kana kwamba simu kutoka kwa maafisa wa ngazi za juu zilikuwa zikichelewesha mchakato wa kusajili chama,” alisema.

Chama hicho baadaye kilisajiliwa na kubadilisha jina kuwa Linda Mwananchi Movement (LMM) baada ya kuidhinishwa kwa kauli moja katika mkutano wa wajumbe Novemba 13, 2026.

Profesa Kefa Otiso wa Chuo Kikuu cha Bowling Green State alisema mchango mkubwa wa Wakenya wanaoishi ughaibuni kwa wanasiasa ni kuchangisha fedha na kuwashawishi jamaa na marafiki walio nyumbani kuwaunga mkono wagombeaji.

“Fedha kutoka ughaibuni zimekuwa muhimu kwa sababu Wakenya wanaoishi huko wana uwezo wa kuchangia kiasi kikubwa. Nchini Kenya, wanasiasa huwapa wapigakura fedha, lakini ughaibuni Wakenya huchangia wagombeaji,” alisema.

Mtandao wa LMM nchini Amerika umeunda matawi katika majimbo yote 50.

In brief

WAKENYA wanaoishi Amerika wanatazamia kwa hamu ziara ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, ambaye anatarajiwa kuwasili nchini humo huku akijipanga kuimarisha uungwaji mkono wake kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. “Fedha kutoka ughaibuni zimekuwa muhimu kwa sababu Wakenya wanaoishi huko wana uwezo wa kuchangia kiasi kikubwa. Nchini Kenya, wanasiasa huwapa wapigakura fedha, lakini ughaibuni Wakenya huchangia wagombeaji,” alisema.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.