📰 Newspapers

Ripoti: Magenge 309 ya uhalifu yatishia usalama nchini

Ripoti: Magenge 309 ya uhalifu yatishia usalama nchini

BONDE la Ufa, Pwani na Nairobi ndiyo maeneo yanayoongoza kwa idadi kubwa ya magenge ya uhalifu yanayotishia usalama wa wananchi, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyowasilishwa bungeni na Rais William Ruto.

Ripoti kuhusu hali ya usalama nchini inaonyesha kuwa kuna jumla ya magenge na makundi 309 ya uhalifu kote nchini, ingawa baadhi yake hayafanyi shughuli kwa sasa.

Idadi hiyo imeongezeka kwa makundi 200 ikilinganishwa na mwezi uliopita, wakati serikali ilipotangaza kuwa ilikuwa imetambua magenge 109.

Mwaka 2016, kupitia Tangazo la Serikali Na. 10427, magenge 89 yalitangazwa kuwa haramu.

Ripoti hiyo inayohusu kipindi cha Septemba 2025 hadi Agosti 31, 2026, inaonyesha kuwa Bonde la Ufa linaongoza kwa magenge 20 yanayotekeleza shughuli za uhalifu, likifuatiwa na Pwani iliyo na magenge 17, Nairobi 11, Magharibi 10, Nyanza saba, Mashariki manne na Kati matatu.

Baadhi ya magenge yanayofanya shughuli Bonde la Ufa ni Watizedi, Kamiti, Confirm, Barsuliek, Cheptiret Boys, DNA, Answi, Chafua, Exodus na Isilando.

Pwani kuna Empire, Military Gang, Wakali Wao, Kitimboni, Zoza Nation, Team Mashamba, Mombasa Republican Council (MRC), Panga Boys na Mawoza.

Katika Nairobi kuna magenge kama Team Kazoo, Mujahedeen, Matopeni Mafia, Jeshi ya Allah, Mbogi Genje, Gaza, Tokyo Mafia na Team Mbogi.

Magharibi kuna Border Defence Force, Bogi Mawe, Jobless Gang, Marachi Republican Council na Fimbo Movement, huku Nyanza kukiwa na Darfur, China Squad, Sungusungu, Chinkororo na Katalang.

In brief

BONDE la Ufa, Pwani na Nairobi ndiyo maeneo yanayoongoza kwa idadi kubwa ya magenge ya uhalifu yanayotishia usalama wa wananchi, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyowasilishwa bungeni na Rais William Ruto. Ripoti kuhusu hali ya usalama nchini inaonyesha kuwa kuna jumla ya magenge na makundi 309 ya uhalifu kote nchini, ingawa baadhi yake hayafanyi shughuli kwa sasa.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.