📰 Newspapers

Makanisa yageuza tohara ya wavulana kuwa biashara nono

Makanisa yageuza tohara ya wavulana kuwa biashara nono

KWA miaka mingi, tohara ilikuwa jukumu la wazee waliokuwa na mamlaka ya kuamua wakati, mahali na jinsi wavulana walivyopaswa kutahiriwa.

Lakini sasa makanisa yamechukua nafasi hiyo, yakigeuza utamaduni uliorithishwa kutoka kizazi hadi kizazi kuwa shughuli inayohusisha malipo ya maelfu ya shilingi.

Miezi ya Novemba na Desemba, familia katika maeneo ya Bonde la Ufa na Mlima Kenya humiminika katika makanisa kuwaandikisha wana wao katika kambi za tohara zinazochanganya matibabu, mafundisho ya Kikristo na mafunzo ya maisha.

Badala ya kwenda msituni au kwenye vituo vya kitamaduni vilivyoendeshwa na wazee, wavulana hukaa katika kumbi za makanisa kwa siku saba hadi 14, wakihudumiwa na madaktari na walezi.

Wazazi hulipa kati ya Sh10,000 na Sh50,000 kutegemea kanisa, eneo na muda wa kambi. Kwa hivyo, tohara imegeuka kuwa biashara ya msimu inayozalisha mamilioni ya shilingi kila mwaka.

Mlezi wa kitaifa wa Baraza la Wazee wa Kikuyu, Kiama Kia Ma, Kung’u Muigai, anasema wazee wamepokonywa jukumu lao muhimu katika jamii.

“Watu hawaliiti biashara, wanaliita huduma ya kanisa,” anasema, akiongeza kuwa shughuli hiyo sasa ina thamani ya mamilioni ya pesa kila mwaka.

Kwa mujibu wa Joseph Kaguthi, mratibu wa wazee na viongozi wa dini katika Baraza la Pamoja la Wazee wa Mlima Kenya, tohara ilikuwa chini ya usimamizi wa wazee.

Wao ndio walioamua nani angefanya tohara, lini na wapi, huku wavulana wakifundishwa majukumu yao katika jamii na kujiunga…

In brief

KWA miaka mingi, tohara ilikuwa jukumu la wazee waliokuwa na mamlaka ya kuamua wakati, mahali na jinsi wavulana walivyopaswa kutahiriwa. Kwa hivyo, tohara imegeuka kuwa biashara ya msimu inayozalisha mamilioni ya shilingi kila mwaka. Kwa mujibu wa Joseph Kaguthi, mratibu wa wazee na viongozi wa dini katika Baraza la Pamoja la Wazee wa Mlima Kenya, tohara ilikuwa chini ya usimamizi wa wazee.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.