📰 Newspapers

Hapa ni kuchimbana? Mrengo wa upinzani, ndani ya upinzani waibuka

Hapa ni kuchimbana? Mrengo wa upinzani, ndani ya upinzani waibuka

SIASA za upinzani zimepata sura mpya baada ya vigogo wanne, Fred Matiang’i, Ndindi Nyoro, Martha Karua na James Orengo kuonekana wakishirikiana katika juhudi za kuunda mrengo mpya wa kisiasa unaoweza kuathiri mikakati ya kumuondoa Rais William Ruto madarakani mwaka 2027.

Muungano unaochipuka wa viongozi hao umeanza kuvutia hisia za kisiasa, hasa baada ya kufanya ziara ya pamoja katika eneo la Gusii, huku wakitarajiwa kuelekea Kirinyaga leo, nyumbani kwa Bi Karua, kwa mikutano mingine ya kisiasa.

Ingawa viongozi hao wanasisitiza kuwa lengo lao ni kupanua wigo wa upinzani kote nchini, hatua zao zimeibua maswali kuhusu iwapo wanajenga muungano mpya ndani ya upinzani au wanajiandaa kuwania nafasi kubwa katika mazungumzo yatakayoamua mgombeaji wa urais wa upinzani.

Baadhi ya watu wa karibu na viongozi hao wanasema ushirikiano huo umechochewa na kile wanachokitaja kuwa uongozi wa mabavu wa baadhi ya vinara wa upinzani, ambao wanahofia unaweza kudhoofisha juhudi za pamoja za kumkabili Dkt Ruto.

Mvutano huo unajiri wakati ambapo upinzani bado unakabiliwa na changamoto ya kuafikiana kuhusu uongozi na mgombeaji mmoja wa urais.

Utafiti wa hivi majuzi wa kampuni ya TIFA unaonyesha kuwa asilimia 43 ya waliohojiwa wanamtaja aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kuwa kikwazo kikubwa zaidi kwa umoja wa upinzani.

Rais Ruto anafuata kwa asilimia 15, huku kiongozi wa vuguvugu la Linda Mwananchi Edwin Sifuna akipata asilimia saba na kiongozi wa Wiper Kalonzo…

In brief

SIASA za upinzani zimepata sura mpya baada ya vigogo wanne, Fred Matiang’i, Ndindi Nyoro, Martha Karua na James Orengo kuonekana wakishirikiana katika juhudi za kuunda mrengo mpya wa kisiasa unaoweza kuathiri mikakati ya kumuondoa Rais William Ruto madarakani mwaka 2027. Ingawa viongozi hao wanasisitiza kuwa lengo lao ni kupanua wigo wa upinzani kote nchini, hatua zao zimeibua maswali kuhusu iwapo wanajenga muungano mpya ndani ya upinzani au wanajiandaa kuwania nafasi kubwa katika mazungumzo yatakayoamua mgombeaji wa urais wa upinzani.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.