📰 Newspapers

Kiti cha naibu rais chazua ushindani mkali 2027 katika serikali na upinzani

Kiti cha naibu rais chazua ushindani mkali 2027 katika serikali na upinzani

VITA vya kuwania unaibu rais vimeanza kushika kasi katika kambi za Rais William Ruto na upinzani unaoongozwa na aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagua, huku viongozi mbalimbali wakimezea mate wadhifa huo muhimu katika uchaguzi wa 2027.

Katika serikali, Naibu Rais Kithure Kindiki anakabiliwa na ushindani kutoka kwa viongozi wa Mlima Kenya wanaotaka kuchukua nafasi yake.

Miongoni mwa wanaotajwa ni Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru, Mbunge wa Ndia George Kariuki, Kiongozi wa Wengi Kimani Ichung’wah na Mwangi Kiunjuri wa chama cha TSP.

Hata hivyo, washirika wa Kindiki, akiwemo Gavana wa Nakuru Susan Kihika na Mbunge wa Nakuru Town East David Gikaria, wanasisitiza kuwa anafaa kuendelea kuwa mgombea mwenza wa Dkt Ruto.

Kwa upande mwingine, chama cha ODM pia kinataka kushirikishwa katika mazungumzo ya kugawana mamlaka kupitia ushirikiano wake na UDA.

Viongozi wanaotajwa kuwa na nafasi ni Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga, mawaziri Hassan Joho na Wycliffe Oparanya.

Utafiti wa TIFA uliofanywa kati ya Oktoba 26 na Novemba 5 ulionyesha kuwa asilimia 55 ya wafuasi wa Dkt Ruto wanamuunga mkono Profesa Kindiki kuwa mgombea mwenza. Wanga alipata asilimia 12 huku Joho akipata tisa.

Hata hivyo, utafiti wa Swiss Poll International uliotolewa Oktoba 28 ulimweka Waiguru mbele kwa asilimia 43, akifuatiwa na Kindiki kwa asilimia 30 na Wanga kwa asilimia 13.

In brief

VITA vya kuwania unaibu rais vimeanza kushika kasi katika kambi za Rais William Ruto na upinzani unaoongozwa na aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagua, huku viongozi mbalimbali wakimezea mate wadhifa huo muhimu katika uchaguzi wa 2027. Katika serikali, Naibu Rais Kithure Kindiki anakabiliwa na ushindani kutoka kwa viongozi wa Mlima Kenya wanaotaka kuchukua nafasi yake. Wanga alipata asilimia 12 huku Joho akipata tisa.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.